Ujumbe huu ni Sehemu ya Kitabu Chetu Kipya cha MOTO WA UAMSHO KATIKA BIBLIA (Tunachambua kila Kila Tukio Lenye Uamsho ktk Biblia Nzima).
Na Mwl Oscar Samba
Kitabu cha Kutoka ... na Yoshua Sura ya 3 na 4, pia Yohana 2:7-11.
Somo la ....: Ishara na Miujiza Kwa Mkono wa Musa: MIUJIZA HUITAMBULISHA HUDUMA.
Shalom mtu wa Mungu, tumekutana tena katika somo jingine. Hapa kwa pamoja tunaangazia nafasi ya ishara na miujiza katika kuitambulisha huduma au mtumishi husika.
Tukiwa tungali katika wito wa Musa kwenye kitabu hiki cha Kutoka; Musa alipoitwa, na kukabidhiwa majukumu kadhaa, alionyesha hali ya kutokukubalika. Alikuwa na mashaka au wasiwasi kama atapata kibali kutoka kwa watu. Jibu la Mungu lilikuwa ni jepesi tu kwake, Mungu alimpatia ishara kadha wa kadha. Na kumwambia ya kuwa, watamuamini kwa kupitia hizo.