Jumamosi, 10 Januari 2026

Mfululizo wa 7, Katika Kitabu Chetu cha CHAKUFANYA UKIWA NJIA PANDA, Pointi ya 4.

Na _Mwl. Oscar Samba_ 

 4. Tafuta Ushauri Sahihi.

Hapo juu nimekupa mfano wa huyu baba ambaye alifikia mahali

pagumu sana kimaamuzi, ila mkewe alimshauri asimwache Mungu.

Badala yake waombe, nukuu moja wapo inamtaja au inamkariri huyu

baba akiwa anasema kuwa, Mungu amempa mke mzuri sana maana

alimshauri vyema!


Katika nyakati kama hizi ni muhim kujua umhimu wa namna ya

kukabiliana na shauri mbalimbali, maana wapo marafiki wataabishaji

ambao hawataacha kuja kwa nia ya kukuyumbisha kiushauri.

Kwenye fikra zako ni alzima kuwa na akiba ya hekima na maraifa ya

namna ya kukabilina na mamabo au amsuari au hali amahizi;

Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na

utimilifu wako? Umkufuru Mungu, ukafe.

Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao

wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa

Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu

hakufanya dhambi kwa midomo yake. Ayubu 2:9-10

Kuna watu wamejikuta wakikwama kwa sababu tu ya kutekeleza

ushauri mbovu. Wameoa na kuolewa nje ya mpango wa Mungu,

ameanguka ili tu wapate watoto. Maana mwenzake kapoteza uwezo wa

uzazi, ama ili tu apate kazi! Yaani kwake ni bora apate kazi lakini

ampoteze Yesu. Kwake mtoto ni wa thamani kuliko uhusiano wake na

Mngu! Najua ni pagumu ila lazima uwe tayari kuingia gharama yoyote

kwa ajili ya Kristo. Najua ni vigumu ila kumfuata Yesu kuna gharama

zake mpendwa! Na jaribu sio jaribu hadi limekuacha njia

panda; hadi ufikie hatua ya kuamua Yesu au Njia Nyingine

Ndipo Huwa Jaribu. Nje ya hapo ni Changamoto ya

Kawaida Tu! Ukiona umefikia hatua ya kuamua au eneo

ambalo unalopaswa kuamua aida Yesu au Njia ya Mkato,

uwe na hakika hapo sasa umefika kwenye jaribu!

Mtoto wa mfalme Sulemani alikwamishwa na ushari mbovu.

Alipotekeleza shauri la vijana ambalo lilikuwa baya, alijikuta anaugawa

ufalme alioachiwa na babaye! Sijui katika njia panda yako kama huwa

unajiombea ili uweze kutambua uwepo wa Mungu au roho nyingine

ama ubinadamu katika aina ya mashauri yanayokuzunguka!

Maana kipindi kama hiki adui hushambulia sana uwezo wako

wakufanya maamuzi! Na kadri mashauri yanavyozidi kuwa mengi

ndivyo na nafsi yako huwa katika mazingira magumu zaidi ya kumua.

Husasani kama mshauri hayo ni njia mbalimbali, maana hata waswahili

husema kuwa miluzi mingi humpoteza mbwa.


Maana anaitwa huku, anaitwa kule, hajui pa kuelekea! Ila mbwa makini

atatulia, na kukaa hapohapo au kando ya njia. Akitaka kujua ni ipi sauti

ya bwana wake, ni ipi sauti ya anayemtunza! Ni ipi sauti ya

anayemlindia nyumba yake! Na akiijua huifuta. Maana itakwepo, na

kama haipo atatatumbua bwana wangu sio miongoni mwa wanaoniita.

Kwa hiyo atatulia au ataendelea na pilika-pilika zake na hatafuata njia

ya sauti yoyote ile! Kujifunza kutaka kumjua Mungu, au kulitaka shauri

ama ushauri wake ni muhimu sana katika nyakati kama hizi.


Usipitwe na Ule Ujao Wenye Pointi ya TAFUTA MAPENZI YA MUNGU..


Yamkini Hujaokoka, na Unawiwa Moyoni Mwako Kufanya Vivyo... Tafadhali Fuatisha Pamoja Nami Sala Hii ya Toba..


Sema; MUNGU BABA, NINAKUJA MBELE ZAKO, MIMI NI MWENYE DHAMBI NAKUOMBA UNISAMEHE SASA; Amen.


Kipakue Bure Kitabu Hiki Google


Tafadhali Tafuta Kanisa la Watu Waliokoka Ukasali Hapo..

WhatApp, Tufolo; https://whatsapp.com/channel/0029Va827LBJENy9u6Enke1h


Kwa Maombi: +255759859287 

http://www.ukombozigospel.blogspot.com

Tumeunda Channel ya 

Kundi letu la WhatsApp https://chat.whatsapp.com/E0eD0xegh1eIGMjRykPyRD

Telegram https://t.me/+fft3GHXC9xIzYjhk

Subscribe YouTube yetu: https://www.youtube.com/@ukombozigospeltv

Kwa Maombi +255759859287 

Usiache Kutembelea na Ku-Like Page Yetu Ya Mafundisho ya Neno la Mungu Facebook: https://www.facebook.com/MafundishoyanenolaMungunamwalimuoscarsamba?mibextid=ZbWKwL


UWE NA AMANI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni