Utangulizi wa Kitabu Chetu Kipya Cha_ Jifunze Kumuamini Roho Mtakatifu Katika Eneo Hilo ....
Na Mwl. Oscar Samba
Utangulizi
Tumekuwa na utamaduni mkubwa sana wa kutegemea akili zetu bila kufahamu umuhimu wa kumtegemea Roho Mtakatifu. Ni kweli akili na fahamu zetu ni kiungo muhimu katika kuyaendesha maisha yetu. Ila Kibiblia mwanadamu hakuumbwa kuzitegemea, badala yake aliumbwa kumtegemea Mungu, ingawaje aliumbwa kuzitumia akili; tena Paulo mtume anamtaka azitumie ipasavyo. Kwake sio kuzitumia tu, bali ni ipasavyo. Utafiti mmoja rasmi uliwahi kuonyesha kuwa, bara fulani ulimwenguni watu wake tunatumia asilimia tano tu ya ubongo wetu. Natumai hii ni sehemu au chachu kubwa ya hali duni ya maisha tuliyonayo.
Lakini tena na tena, yote katika yote; ni kwamba akili za mwanadamu ziliumbwa zifanye kazi kwa msaada wa Kiungu. Ni dhambi tu ilivuruga eneo hili, na kumfanya mwanadamu kuishi kana kwamba
alijiumba, au hakuna aliyebeba ramani ya maisha yake. "Solo life" yaani maisha ya kujiongoza, yalianzia Edeni kama matokeo ya dhambi.Sulemani mtu aliyejawa na hekima nyingi, kiongozi na mtu tajiri sana katika zama zake, alitupa somo hili la kutokuzitegemea akili zetu. Ingawaje, kati ya watu wanaoonya kuhusu ujinga na upumbavu ni yeye, kati ya wanaotusihi kuwa na hekima na busara na akili ili tufanikiwa maishani: bado ni yeye.
Ila hapa anatupa muongozo muhimu sana; Mithali 3:5 Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; 6 Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.
Anatutangulizia hali ya kumtumaini Bwana kwa moyo wote, anaweka neno "wala" na kukutaka usizitegemee akili. Hajasema usizitumie, bali usiweke tegemeo hapo. Na badala yake umkiri, Biblia ya kingereza ya KJV ikatumia neno la "acknowledge" yaani kutambua utendaji wake kwako kwa njia ya kukiri au kudhibitisha. Sisi tukakwambia katika kiswahili mkiri Yeye, kisha na njia au mapito yako yatanyooshwa...
Hapo tunajifunza kuwa, kumtegemea Roho Mtakatifu, kunakupa kunyooshwa kwa mapito yako. Kumbuka imizo ni kutokuzitegemea akili zako. Kwa hiyo, ukiweka tumaini katika akili, elimu, ujuzi au uzoefu wako; unajitengenezea mazingira ya njia zako kutokunyooshwa. Hali itakayokukwamisha tu.
Kwa hiyo kitabu hiki kinanuia kukusaidia kuona umuhimu wa kumpa Roho Mtakatifu nafasi ya kwanza. Kuweka tumaini lako kwake, nia yangu kuu ni kukufunza umuhimu wa kuweka imani kwake. Kumuamini.
Ninanuia kukusaidia kufahamu na kisha kuelewa ya kuwa njia unayoiendea, Roho Mtakatifu alishaipita. Maana anajua mwisho wake hata kabla ya mwanzo wako. Sasa kama unapita njia ambayo huna uhakika nayo, alafu unakuta a na mtu aliyefika mpaka mwisho akiwa anarudi, huku kichwani akiwa na furushi la kuni hali inayoonyesha wazi kafika hadi msituni eneo lenye kuni unakoelekea wewe: unapata kigugumizi gani kumuuliza hali ya njia hiyo? Kila eneo ambalo una mashaka nalo kuhusu njia utamuuliza hapana shaka, hata lile daraja lililovunjika utataka kujua kama limeboreshwa au kuna namna gani mpya ya kuvuka. Hatari ya wanyama na kadhalika; kwa hiyo, Roho Mtakatifu alishatutangulia, TUMUAMINI YEYE.
Kitabu Kikitoka Tafadhali Kitafute
Na kwa Vitabu km hivi Tuandikie Ujumbe wenye Neno VITABU Wasapu Nasi tutakutumia
Namba: +25559859287
Namba hizo zinaweza tumika kwa sadaka yako pia katika M-Pesa jina ni Oscar Samba
Zaidi Endelea Kutembelea:
https://ukombozigospel.blogspot.com/?m=1
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni