Kuwa Makini, Unapozungukwa na Watu Waliobeba Tochi Inayomulika Ulipokanyaga (Wakitafuta Makosa); Na Sio Wakumulikie Ili Usikosee Kukanyaga.
By Mwalimu Oscar Samba
Kuwa Makini, Unapozungukwa na Watu Waliobeba Tochi Inayomulika Ulipokanyaga (Wakitafuta Makosa); Na Sio Wakumulikie Ili Usikosee Kukanyaga.
By Mwalimu Oscar Samba
Sii Kila Wakati Unahitaji Taa; Kuna Nyakati Unahitaji Macho Yenye Taa.
Jifunze kwa Wanyama Waonao Usiku!
Mwenye Taa, Akikimbia Nayo; Unabaki na Macho Yako: Usiku na Mchana Utaweza Kutembea.
*UTOFAUTI KATI YA MSAADA NA SADAKA*
Nimejibu swali la Mpendwa aliyetaka kujua huo utofauti
1.Msaada unatoa chochote....Sadaka Unatoa Ulichoguswa moyoni
2. Sadaka Unatoa ukiwa na Imani Kuna kitu nitapata kutoka kwa Mungu...Msaada unatoa ili kukidhi tu hitajio
3. Sadaka Unatoa kama kwa Bwana,....Msaada Unatoa kwa kumlenga muhusika
4. Sadaka Ukiitoa kwa Mazoea ina Adhabu kwa Mungu, Kuna kukataliwa kama Kaini au watu wa Kitabu cha Malaki moja na mbili...ila Msaada Sivyo
5. Baraka za Sadaka ni Kubwa kuliko Msaada.
6. Utoaji wa Sadaka Hukukutanisha na Mungu...Mfano Kornerio ktk Mtd. 10, na Mfalme Sulemani; 1 Wafalme 3. .....ila msaada utakutana tu na shukurani za wapokeaji...
NB: (a). Unaweza Kugeuza Msaada Kuwa Sadaka kwa Kuliombea jambo hili ili utoaji wako uwe na mguso wa Kiungu.
(b). Pia Kusikia Moyoni Mwako Roho Anakusukuma Kutoa nini?
(c) Toa Kwa Imani...yaani tarajia kitu kutoka kwa Mungu.
Muhimu : Kama ndivyo basi, likija changizo lolote, ikiwemo la harusi au kanisani...usiwe mwepesi kutoa kiwango kile kile kilichoainishwa au kuombwa kwenye kadi au kile cha desturi.
Badala yake tenga muda wa kutaka mapenzi ya Kiungu hapo. Sii vibaya ukavuka lengo lao au mazoea, kusikia kutoka moyoni na kutii ndiko kutakakobadili utoaji huo kutoka kwenye mchango au changizo la kawaida na kuwa Sadaka.
Maana Warumi 10:17 hutuambia imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huko huja kutokana na Neno la Kristo na neno ni Kristo Mwenyewe...na utoaji wa kiimani ndiyo huitwa Sadaka.
Ukichunguza kwa umakini ujumbe huu...utagundua ya kuwa hata makanisani muda ule wa sadaka wengi wetu hatutoi Sadaka bali ni kama msaada.
Tunatoa kwa sababu bila hivyo mchungaji ataishiwa chakula, tunatoa kwa sababu jirani yangu hapa atanionaje nimekuja kanisani bila Sadaka! Ama ninaona aibu wenzangu wote wamesimama kutoa na mimi sijatoa!
Tunachangia kwa sababu bila hivyo kengo halitajengwa...! Ni kweli ni wajibu...lakini badili wajibu kuwa Imani..
Ndiyo maana watu wengi ni wagumu kutoa kwenye ujenzi wa kanisa jingine, tena kama ni dhehebu tofauti basi ndipo huwa wagumu zaidi.
Sababu kubwa ni imani kukosekana katika hili. Moyo wowote wa utoaji, lazima daraja lake liwe ni imani. Licha ya imani kutarajia kutoka kwa Mungu...lakini kitu kimoja wapo kikubwa inafanya ni kuyataka mapenzi ya Mungu katika hilo jambo...Kumsikia Yeye na Kumtii.
Maandiko yanaposema kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, hunuia kutusaidia katika kusudio lililozaliwa na imani. Ndiposa anatukumbusha kuwa akitoa haba au kidogo atapata kidogo, na baraka zipo kwa anayetoa kwa moyo wa ukarimu...huu sio ukarimu wa kawaida ni ukarimu ambao ndani yake una nasaba za Kiungu....
Note : Kilio kikubwa cha kutoa sana na kutokuziona baraka...kinatokana na imani kutokuwa daraja la utoaji....utoaji ukiunganishwa na daraja la mazoea, msaada, changizo na hata lile la ninaona aibu wenzangu wanatoa mimi sijatoa; uwe na hakika baraka zake ni haba au hafifu.
Mungu anaposema atoaye haba atapata haba, ni makosa kulitazama hili andiko kwa kuangalia kiwango cha utoaji tu...Mungu hakuwa analenga tu kiwango cha utoaji...maana yule mwanamke alitoa kidogo kwa jinsi ya kipimo, ila kwa Mungu hakikuwa haba.
Imani ni kitu muhimu sana kinachopimwa hapo...utaiona kwa yule mwanamke wa kipindi cha Yesu, imani ilimsukuma kutoa vyote!
Huwezi kutoa vyote kama huna tarajio na humuamini aliyekutaka kutoa ya kwamba hatima ya maisha yako yote anayo yeye!
Ni rahisi kutoa ziada, au kumi ya 100 kati ya vile ulivyo navyo, maana una uhakika jioni asilimia 90 iliyosalia itakulisha, italipa yamkini na ada pia na hata rejesho la VICOBA!
Ila kutoa vyote, yaani asilimia 100 yote, ni imani kubwa sana maana umemuachia Mungu chakula cha jioni, ada na rejesho.
Sikuimizi kufanya hivyo!
Maana pia kama hujasikia kutoka moyoni bado itakuwa sio imani ni msisimko!
Na hapa ndipo wengi wanakwama...wanatoa kwa msisimko na wanashangaa hawajapokea hadi leo!
Imani lazima izaliwe katika kusikia ndani!
Tatizo wengine ni viziwi wa kiroho, masikio yao kwenye utoaji yamezibwa...hata Roho Mtakatifu akisema hawasikii....unapaswa kutatua hili tatizo...
By Mwalimu Oscar Samba
Kuna Watu Ukiwaambia "Mimi ni Big Brain," Watakuuliza "Do You Have Any Article?" Na Wengine Watakutazama Umevaaje!
#Vijana Wengi Wameamua Kuwa Kundi la Pili.
By Mwalimu Oscar Samba
Tatizo Kubwa la Viongozi wa Kiafrika Sio Kukosa Maono; Ni Kushindwa Kupandikiza Maono Kwa Watu Wanaowaongoza. Hawajui Hakuna Mkuu wa Jeshi Anayeshinda Vita Kutokana na Uwezo Wake Binafsi tu; Bali ni Kwa Sababu Amefanikiwa Kuandaa Jeshi Zuri. Ubora wa Kocha Unapimwa Kutokana na Uwezo Wake wa Kuandaa Timu Nzuri.
Ukifeli Kuwafanya Wafikiri Kama Wewe, Uwe na Hakika Watafikiri Kama Wao; Na Watatenda Kiholela.
By Mwalimu Oscar Samba
Gharama Moja Wapo ya Kulea Ni Kuvumilia, Kujifunza Kumchukulia na Kuchukuliana Huku Ukisalia Katika Lengo na Kusudi la Kutaka Chombo Unachokitaka.
Ni Hatari Kuhitaji Mtu Unayemtaka Awe Unayemtaka Kwa Dakika Moja. Jifunze kwa Fundi Muwashi au Mfinyazi wa Vyungu, Tazama Inavyochukuwa Muda Kukipata Anachokitaka!
Ghrama Kubwa ya Kulea Ipo Kwako Wewe na Sio kwa Anayelelewa; Ustaimilivu na Hekima Vitakusaidia.
Paulo Mtume Hakaanguka Juu ya Mti, Hakujilea...Alilelewa...Wakati Hanania Anasema ni Muuaji, Mungu Alimuona Kuwa Chombo Kiteule..
Unahitaji Jicho la Tatu ili Uweze Kuondokana na la Pili Linalomuona Sauli Muuaji; La Tatu Litamuona Chombo Kiteule.
John Marko Alionekana Hafai, Barnaba Alimuona Anafaa Katika Kipindi Ambacho Alikuwa Hafai.
Ni Muhimu Pia Kuwaheshimu Waliokuona Unafaa Katika Majira ya Ulipokuwa Hufai; Maana Sasa Kila Mtu Anakuona Unafaa kwa Saabu Unawafa; Fahamu Yupo Aliyelipa Gharama.
Ni Kweli Utukufu ni kwa Mungu. Lakini Kumbuka Alimtumia Barnaba Kumuandaa Sauli Aliye Paulo na John Marko.
NB: Tatizo la Sasa sio Wakina John Marko na Wakina Paulo Wanaotufaa Katika Utumishi; Ila Tatizo ni Kukosekana kwa Walezi Wenye Fikra za Ukocha...Walezi Wengi Wana Fikra za Ushindi, Yaani Wamtumie Nani ili Wafanikiwe na Sio Wamuandae Nani ili Wafanikishe Malengo yao. Asante:
"Ukishindwa Kulea, Ni Umeshindwa Kurithisha; Kwa Hiyo Jiandae Kusahaulika."
By Mwalimu Oscar Samba
www.ukombozigospel.blogspot.com
Nina *Mshukuru Mungu* kwa Kufanikiwa Kukamilisha Kitabu Changu Kipya cha Uchambuzi wa Kitabu cha Matendo ya Mitume. Kitabu kinaitwa SIRI YA *MAFANIKIO KWA KANISA LA KWANZA* ( *kanisa la Mitendo ya Mitume) By Mwl Oscar Prospa Samba mwana wa Flora Samba
Kipakiwe Bure Kitabu hiki Free Download Pdf
Bonyeza Hapa Mwalimu Oscar Samba SIRI YA MAFANIKIO KWA KANISA LA KWANZA (Kanisa la Matendo ya Mitume)
Felix Mbwanji:
SAMEHE NA KUSAHAU (BY MWL, C.MWAKASEGE)
TABIA YA MUNGU YA KUSAMEHE NDANI YAKO
Ulipompokea Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako, ulipokea tabia ya aina gani?
" Bali wote waliompokea (Kristo) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu." (Yohana 1:12,13)
Ulipozaliwa mara ya pili kwa Neno la Kristo ulifanyika kuwa mtoto wa Mungu.
Watoto wa Mungu wana tabia ya namna gani?
Kwa kuwa wamehamishwa toka ufalme mwingine na uzazi mwingine, na kuingizwa katika ufalme wa Mungu na uzazi wake (Wakolosai 1:13); watoto hawa wanatakiwa wawe na tabia nyingine.
Kabla ya kuzaliwa mara ya pili, kabla ya kumkiri Kristo ya kuwa ni Bwana: ulikuwa na tabia ya dunia hii iliyoongozwa na mfalme wa dunia hii ambaye ni shetani.
Ulipozaliwa mara ya pili na kuukiri wokovu katika Kristo, ulipokea tabia mpya inayoongozwa na Mungu mwenyewe aliye ndani yako.
" Kwa kuwa uwezo wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa (Utakatifu), kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno; za thamani,ili kwamba kwa hizo mpate kuwa Washirika wa TABIA YA UUNGU, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa." (2 Petro 1:3,4)
Na Christopher Mwakasege_
Leo nataka tujifunze juu ya “Mwongozo wa kutafakari na kuombea ndoto zenye UZINIFU AU UASHERATI ndani yake”.
Maneno haya ‘uzinifu na uasherati’ yanahusu ufanyikaji wa tendo la ndoa usio halali kibiblia. Uzinifu linatumika zaidi wakati tendo la ndoa limefanywa na mtu ambaye hajaoa au hajaolewa. ‘Uasherati’ linatumika zaidi wakati tendo la ndoa limefanywa nje ya ndoa na mtu ambaye ameoa au ameolewa.
Mtu anayepata ndoto zenye mambo hayo, huwa zina madhara makubwa sana ya kiroho, na ya kimwili – kwa aliyeota ndoto hizo!
Kumbuka kwamba: Neno la Mungu la biblia, kwa kushirikiana na Roho Mtakatifu, linatuongoza kujua namna ya kutafsiri na kuziombea ndoto za aina yo yote – ambazo ni pamoja na hizi zenye mambo ya uzinifu au uasherati ndani yake.
Mwl OSCAR SAMBA ( #NasahazaMwlOscar )
#FaidayaJaribu: #Usiogope
Na Mwl. Oscar Samba
Kwenye Kipengele cha Faida za Uzima wa Milele
2. Tunakula Matunda ya Mti wa Uzima. Huu ni mti wa ajabu sana. Kumbuka mti huu ndio uliowafanya Adamu na mkewe kuondolewa kwenye bustani ya Edeni. Mimi na wewe leo hatupo hapo bustanini kwa sababu ya hii dhambi.
Mungu alihofia wasije wakala na kisha wakaishi milele.
Ufunuo wa Yohana 2:7 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu. (Nikutie moyo pia kuhakikisha unashinda vita, majaribu, maana mbingu ni mji wa washindi! Sio sehemu ya walioshindwa! Hili lijue na ulifikiri daima maana ni taswira halisi unayopaswa kuwa nayo kwenye fahamu zako.)
Tujione Siri hii muhimu kule Edeni:
Mwanzo 3:22 Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele; 23 kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa.
24 Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.
Kilichowafanya kuondolewa sio uzuri wa bustani! Sio kwamba wameshafanya dhambi kwa hiyo hawastaili tena kuendelea kula mema ya hiyo bustani, la! Bali ni kwa sababu ya uwepo wa huu mti. Ndiyo sababu kubwa Mungu anayoitoa anapowaondosha hapo.
Na Mwl Oscar Samba
#FaidayaJaribu: #Usiogope
Ni Sehemu ya Kitabu Chetu Tarajiwa cha MAANA YA UZIMA, NA UZIMA WA MILELE. Pwenti ya Pumziko Kuu.
Kwenye Kipengele cha Taswira ya Uzima wa Milele
Pumziko Kuu; Yaani Sabato Kukuu. Watu wengi hawajui ya kuwa Sabato maana yake ni pumziko katika kilele cha uzima wa milele yaani wakati huu hapa ulimwenguni kwa kuokoka, (kupumzika katika Kristo Yesu kama mtua mizigo ya dhambi na kila mateso.) Na pili kama sehemu ya kupumzika kutoka katika dunia iliyopo chini ya umiliki wa Shetani kama mungu wa dunia hii, na pamoja na dunia yenye pigo la laana la kosa la Adamu na Hawa.
Unapookoka ni umeingia katika Sabato. Kwa hiyo, msabato halisi ni mtu aliyeokoka. Kama hujaokoka wewe sio Msabato, maana bado upo chini ya utumwa wa Shetani. Wokovu unakupa pumziko. Kanuni na sheria zile za Agano la Kale hususani sabato na taratibu zake zote, zilinuia kutufikisha hapa kwenye wokovu na hatimaye katika Sabato kamilifu ile ya Mbingu Mpya na Nchi Mpya.
Ndiposa Yesu alipokuja, mkazo wa sheria za kisabato ule wa Agano la Kale haukwepo tena. Maana amekuja Sabato Mwenyewe. Ndio maana alijibu hivi; Marko 2:27 Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato. 28 Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia. ( Kwa hiyo kama utaendelea kusingizia kumsikiliza mjumbe wa Sabato Musa na kumuacha Bwana wa Sabato; basi utakuwa umekwama sana.
Mathayo 12:5 Wala hamkusoma katika torati, kwamba siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi sabato wasipate hatia? 6 Lakini nawaambieni, kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu.
7 Lakini kama mngalijua maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka, msingaliwalaumu wasio na hatia. 8 Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.
Tuone kisa kingine:
Neno la Leo ( #NasahazaMwlOscar )
Neno la Leo ( #NasahazaMwlOscar )