Mwalimu Oscar Samba
Ijumaa, 28 Agosti 2020
Utangulizi wa Kitabu chetu cha UTUMISHI NA MTUMISHI
PENDO LA KRISTO JUU YAKO NI LA MAFANIKIO
Mpendwa nikutie tu moyo kuwa Yesu anakupenda, anakuwazia mawazo yaliyo mema, ni Mawazo ya Amani, Furaha, ana mipango mizuri juu yako, ni Mipango ya Kuinuliwa, Kufanikiwa, kama ilivyo nia yake katika 1 Yohana 3:2, kuwa anataka ufanikiwe kimwili au kifya na katika kila eneo la maisha yako ikiwemo uchumi, ndoa, huduma na kadhalika kama vile roho au nafsi yako ifanikiwavyo:
YESU ANAKUPENDA!
Na Mwalimu Oscar Samba
Sijui kama unajua kuwa Yesu anakupenda! Ni hatari kujaribu kusema kuwa mbona ninateseka, mbona maisha ni magumu, sasa inawezekanaje Yesu anipende wakati huu ni mwaka wa .. sijapona?
Ukweli ni
kwamba Yesu anakupenda, na kuteseka kwako ni wewe tu bado hujatambua unachotakiwa
kufanya ili kukubaliana na pendo hili! Unajua ndugu yangu acha nikwambie ukweli
huu, nikuweke wazi katika viwango hivi vya uwazi! Mungu ili afanye kazi kwenye
maisha yako ni lazima wewe umpe nafasi!
Mungu ni
tofauti sana na Shetani, Shetani huweza kulazimisha, anaweza kutumia hila na
mbinu batili ili kufanya jambo kwenye maisha yako, ila ili Mungu akusaidie wewe
unapaswa kumruhusu!
Mfano, kuna
mama mmoja alitokwa na damu kwa muda wa miaka 12; kwenye biblia tunajuzwa hili
jambo, muda wote huo alikuwa akiwaendea waganga wa kienyeji na matatibu wa dunia
hii! Ila siku alipoamua na kudhamiria moyoni mwake kwa kulishika pindo la vazi
la Yesu hapo hapo alipokea uponyaji, wake!
Sasa jionee!
Ni kwamba kupona kwake, kulitokea pale ambapo aliamua, alidhamiria kumuendea
Yesu; Luka 8:43 Na mwanamke mmoja,
ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa
mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote, 44 alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi
lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma.
Hapo pendo la
Kristo linadhibitika ndani yake! Uponyaji unatokea, lakini sio kwamba Yesu
alianza kumpenda alipomponya la! Upendo ulikwepo ila huyu mama alipoamua
kukubaliana na pendo hilo ndipo alipopona!
Yesu
alitupenda na alimpenda huyu mama hata kabla hajavaa mwili yaani hajaja humu
ulimwenguni, na pendo hili linadhibitishwa na Uungu wote; Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda
ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali
awe na uzima wa milele.
Dhambi
ilipoingia ulimwenguni pendo la namna hii ililijidhiirisha mara! Halikuanzia
katika kuzaliwa kwa Yesu, bali hata Agano la mlima Sinai ni ishara ya hili
pendo, Mungu alipochinja mnyama na kuwavika wakina Adamu nguo ilikuwa ni sehemu
ya utendaji wa hili pendo! Mahali pengine kwenye biblia hujulikana kama neema,
unapoona neema, uwe na hakika huwakilisha pendo la Kristo, tumeokolewa kwa
neema tu, ama tumeitwa kwa neema tu, uwe na uhakika ni pendo lake!
Pendo hili haliwezi
kujifunua kwako wakati ukiwa na shida unaenda kwa waganga wa kienyeji, ukiwa na
mahitaji humulezi Yesu unawaeleza watu tu na kuishia hapo! Hutaki kwenda
kanisani, maana huyu mama alimfuata Yesu kwenye kusanyiko, na penye kusanyiko
maana yake ni penye uwepo wa Mungu, sasa kwenye ibada ndipo alipo Kristo!
Usiende
kanisa ni kanisa, usiende kusanyiko ni kusanyiko, maana siku hizi watumishi
wengi wa uongo wameibuka, tafuta kanisa la watu walio hai kiroho, mahali ambapo
kiukweli hata akili na ufahamu wako wa kawaida unatambua hapo Mungu yupo, epuka
mbwe mbwe za Shetani, na misisimko isiyo na Mungu ndani yake.
Yawe ni
maombi yako na ni maombi yangu pia kuwa Mungu afunguwe macho yako ya ndani ili
uweze kujua sehemu sahihi itakayokuwezesha kukutana na Yesu wa kweli, maana siku
hizi kuna ma-yesu wengi wa uongo, hawamuhubiri Yesu mwenye kukemea dhambi, kwao
dhambi ni sehemu ya ibada, hapo kimbia!
Ukiona huduma
isiyokemea dhambi, hiyo imepotoka, ukiona huduma ambayo wazinzi na walevi wamo
humo humo na ni watumishi, hapo kimbia wala usiage! Ukiona mtumishi anawataka
washirika wake kimapenzi ujue huyo ni “ajenti” ama wakala wa kuzimu, na
ukimkubalia atakuunganisha na kuzimu moja kwa moja, kwani mashariti yao moja
wapo ya kuwaunganisha ni kulala na watu! Hususani wenye nyota ambazo
zitawasaidia kuvuta watu makanisani! Epuka na kimbia hili!
Unajua kuna
watu wanaenda kanisani ili kuirithisha nafsi yao kuwa nao wapo kanisani! Hii ni
hatari sana, ni sawa na kunywa maji machafu ili tu uwe umekunywa maji! Ni sawa
na kula mkapi au vyakula vibovu ili tu kukidhi hitajio la kula! Ukifikia hapo
upo mahali pagumu sana!
Maana baada
ya muda afya yako itakongoroka tu! Wengine huabudu kwa kufuata mkumbo! Yaani ni
mtumishi yupi anawika sana mjini siku za leo, akipoa au akiona ushabiki
umempungua basi hufikiri kuhama hapo! Akiibuka mwingine mjini, humfuata!
Watoto
hata! Shetani huwa naye anahubiri, tena ni muhubiri mzuri tu! Ukipinga muendee
Yesu kwenye Mathayo na Luka 4, utamuona Yesu akihubiriwa na Shetani pale, na maandiko
anamsomea, kuwa akiwa ndie Mwana w aAdamu ageuze jiwe kuwa mkate, na
alimuonyesha hata utajiri alionao akimpa na kanuni kuwa akimsujudia atampatia!
Sasa
usitishike na injili za mafanikio, maana hawakuanza wao alianza Shetani, na
kupata fedha au mafanikio kutoka kwao sio jambo la kigeni, maana hata Yesu angemsujudia
hakika angepewa, maana ni muhimu kujua nao huwa wanamsujudia nani!
Kusoma maandiko
na kuyafafanua siyo kipimo, kwani hata Shetani alimsomea Yesu, maana ni kweli
yapo kwenye biblia! La muhimu na jambo zuri kuliko yote ni wewe kuhakikisha
kuwa ndani yako unapata amani ya Kristo, maana wapo ambao Mungu anawakosesha amani
na mtu husika ila kwa ushabiki huzidi kugandamana naye! Huku ni kupotea!
Injili ambazo
jina la Yesu limewekwa kando, msisitizo wa maombezi sio katika jina la Yesu na
Damu yake kwenye uhalisia, ama nguvu za Roho Mtakatifu, bali ni katika
viambatanishi, au visaidizi, kama mafuta ambayo yamesingiziwa kuwa ya upako, na
wengi hawataki kujua kama ni upako upi unaotajwa hapo, maji ya upako au maji ya
baraka, wengine wanagawa hadi bangili za upako, pete za upako, nasikia siku
hizi kuna keki za upako, hii ni hatari
sana!
Najua wana
wa upotevuni ni wepesi sana kukinzana na ukweli huu, na wana hoja nyingi sana
wakitumia maanadiko, ila mioyoni mwao wanaujua ukweli, maana sifa zipo kwenye
mafuta na maji yakaniponya, Yesu amekuwa kama ni msaidizi!
Nisikilize,
ukitaka kuliona pendo la Kristo likikusaidia maishani mwako ni muhimu sana
kuhakisha kuwa unaambatana na Yesu kama alivyo, waepuke wanaokupa maji machafu,
katika Yohana 7:38-39 Yesu anaita akiwataka wale wenye kiu waje au waende kwake
ili awape maji!
Maji yake ni
safi, alimwambia yule mama kwenye kisima cha Yakobo katika Yohana 4 kuwa
kiyanywa hayo maji ya Yesu hataona kiu tena! Sasa wamekupa Yesu na bado kiu ya
ulevi ipo, wamekupa Yesu na bado una kiu ya kuiba waume za watu! Ukimuona mume
wa mtu mate yanakutoka kama fisi na mfupa! Wamekupa Yesu angali bado una kiu ya
dogo-dogo, ukimuona kijana “handsame” ama binti mrembo, hata kama ni umri wa mwanao
jicho linakutoka kama vile fundi simu aliyedondosha nati, maana nati zake ni
ndogo kwa hiyo asipotoa macho hawezi kuziona kirahisi, huu akiwa na hofu
usikute imepotea!
Unasema eti
umeokoka, au unamependa na una Yesu, sawa sikataii! Lakini mbona hajaondoa kiu
ya dhambi nadani yako! Bado ni mwizi, unazini kwa siri, nyumba ndogo kuacha
umeshindwa! Hakika huna Yesu aliyehai una yesu marehemu! Wala usinikunjie
ndita, ila ukweli ndio huo!
Anasema hivi;
Yohana 4:13 Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji
haya ataona kiu tena.
Yesu
akiingia nadani yako, na kiu ya mambo ya dunia ispoondoka, uwe makini, rejea msalabani
upya!
Neno la
Mungu ni maji, sasa injili kama inahubiriwa haibadilishi maisha yako, kuna mambo
mawili hapo makuu, wewe mwenyewe u na moyo mbovu, ama injili unayopewa ni maji
machafu, ni maji yasiyo na uwezo wa kukausha kiu ya dhambi, na tamaa zake,
swala la upinzani wa Shetani hili ni la maombi tu! Ila hatuwezi au maombi hayawezi
kukusaidia sana kama wewe mwenyewe hujakaa eneo salama, maana pepo mchafu
amtokapo mtu na akipata mwanya mwingine hurejea, maandiko husema mmekuwa safi
kwa lile neno, neno hukuweka kuwa safi, na mapepo hayakai maeneo ambayo
yamesafishwa kwa Damu ya Yesu!
Huwa nasema
kuna yesu aliyekufa, na kuna Yesu aliye hai, unaposema nataka kumuona Yesu,
nina haja na Yesu, uwe makini maana wakina Pilato wapo hapo kukupa yesu
aliyekufa kama Yusufu wa arimathayo, huyu alipewa Yesu/yesu ila mfu,
aliyempatia alihakikisha kuwa amekwisha kufa! Na aina hii ya Yesu hawezi kuleta
mabadiliko kwenye maisha yako!
Unasema una
Yesu lakini hatuoni badiliko la ndani; ndani yako, una sema una Yesu lakini
hatuoni matokeo ya wewe kuhuishwa hata kidogo! Yesu aliye hai, hukushindia
dhambi, huhuisha utu mpya na kuua ule utu wa kale, hawezi kuchangamana na
dhambi! Ukiona unajiita una Yesu lakini hakuna badiliko la dhambi au la kiroho
ndani yako uwe na hakika kuwa kuna shida ipo mahali, utakuwa wamekupa yesu
aliyekufa siyo Yesu aliye hai kama Yule aliyefufuka siku ya tatu, maana kuna
dini zina yesu sawa, ila ni yesu marehemu!
Wanahubiri
habari za Yesu, Lakini wao wenyewe ni wazinzi, ni walevi, hawawezi kusimama
madhabahuni bila kunywa pombe kidogo, hawawezi kukaa bila kutongoza washirika!
Ni mzee wa kanisa ila sigara anavutia chooni!
Ona hapa; Marko
15:44 Lakini Pilato akastaajabu, kwamba
amekwisha kufa. Akamwita yule akida, akamwuliza kwamba amekufa kitambo. 45 Hata alipokwisha kupata hakika kwa yule
akida, alimpa Yusufu yule maiti.
Kuna dini,
zimehakikisha kuwa yesu waliye naye amekwisha kufa, ndio maana wamekupa wewe!
Maji yao siyo yale halisi yenye uwezo wa kuondoa kiu ya dhambi, ndio maana
wamekupa wewe!
Huwa
ninaweka sana angalizo hili, kuwa unapokuwa na kiu ya kutaka kumjua Yesu,
unapokuwa na kiu ya kutaka kukoka, unapaswa kuwa makini tena mno, maana ukisema
nina kiu, moja kwa moja uwe na hakika kuwa wapo watu ambao hawaachi kukuletea
maji, ambayo kwa kweli siyo sahihi, ndio maanaYesu kwenye ile Yohana akapaza
sauti aksema kila mwene kiu na aje kwangu, aje anywe, hakusema na aje achote
maji ila alisema na aje kwangu, kwa hiyo jifunze kumtafuta Yesu kwanza, na sio
maji kwanza , kama wengi wafanyanvyo! (Maana ukiwa na Yesu, atakwambia haya
maji uliyopewa siyo yangu.)
Najifunza
sana kwa Yesu mwenyewe, alipokuwa pale msalabani na alipopatwa na kiu, alisema
naona kiu, na badala ya kumletea maji walimletea siki! Uwe na hakika na wewe
ukisema nina kiu, wapo na watu ambao nao watakuletea siki ama maji machafu!
Ukisema
nataka kuokoka, ninamtaka Yesu watakwambia usiondoke kwenye dini yetu maana na
huku pia watu wanaokoka, kuna vikundi huku nako vya uaomsho, uwe na hakika ni
uamsho bandia, maana kuna na moto bandia, ambao hufananishwa na ule wa Roho
Mtakatifu!
Namtaka
Yesu, wanakuletea Yesu ambaye amekufa, hawezi kuondoa dhambi! Ndio maana adui
ameweka utitiri wa madhehebu na makanisa mapya na watumishi wengi, ni ili kuwapoteza
watu, maana ma-yesu wafu wamejaa sana humu duniani! Umakini unahitajika sana!
Asante kwa
kunisikiliza (nafsini mwako), ama kunifuatilia kwa njia ya usomaji huu wa hii
makala, nina amini kuwa kuna kitu umekipata hapa, Yesu anakupenda, ila kama
hujakutana na pendo lake uwe na hakika kuna dosari ipo mahali, chukua hatua
mapema mnoo!
Pia anasema
kwamba mtu akimpenda atazishia amri zake, kwa hiyo kama kweli umedhamiria,
mpende kwa kuzishika amri zake, epuka michanganyo, epuka kuuzoelea wokovu,
asante na Mungu akubariki mno; Yohana 14:23
Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba
yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. 24 Mtu
asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu,
ila ni lake Baba aliyenipeleka.
Hongera kwa
kusoma ujumbe huu, nakutia moyo kuzidi kumtazama Mungu, na pia uwenda
hujaokoka, yaani Yesu sio Bwana na mwokozi wa maisha yako! Nakutia moyo tena
kuokoka sasa! Yamkini ni uchumi, fedha, hazipatikani, unazingirwa na nuksi na
mikosi, kila unalofanya haliendi, unakabwa na mapepo, ! Wewe njoo kwa Yesu na
hayo yote yatapita kabisa ! Sasa natumi u
tayari!
Sema; MUNGU
BABA, NINAKUPENDA, ASANTE KWA KUNIPENDA KWANZA, LEO NIMETAMBUA KUWA MIMI NI
MWENYE DHAMBI, NA NIPO TAYARI KUOKOOKA, TAFADHALI INGIA NDANI YANGU, SAMEHE
DHAMBI ZANGU, NA FUTA JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKU, NA ULIANDIKE SASA
KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE, Ameni.
Kwa kufanya
hiyo umekwisha kuokoka sasa, na tafadhali tafuta kanisa la watu waliokoka
lililopo karibu nawe ukasali, hapo, waambie kuwa umeokoa hivi karibuni, ili
wakulee vyema kiroho.
Mawasiliano
yetu, kwa M-Pesa au Simu: +255 759 859 287, barua pepe:
ukombozigospel@gmail.com
pia
temnbelea: www.ukombozigospel.blogspot.com
.
Alhamisi, 25 Juni 2020
UWE HODARI, SHUJAA NA MOYO MKUU.
Jumamosi, 20 Juni 2020
Usizike Ndoto Zako.
Alhamisi, 4 Juni 2020
NGUVU YA MAOMBI YA KUOMBA BILA KUKOMA
Ijumaa, 27 Machi 2020
Mwalimu Mwakasege Atoa Wito wa Kushiriki Maombi Dhidi ya Ugonjwa wa Korona
Bwana Yesu asifiwe.
Hili ni ombi kwa kila aliyewahi kuhudhuria kongamano letu,la maombi la kitaifa, tunalofanyia Dodoma kila mwaka. Lakini,hata kama hujawahi kuhudhuria kongamano hilo-ombi hili linakuhusu pia.Tunajua umekuwa ukiombea tatizo la ugonjwa wa 'Corona'. Pamoja
Alhamisi, 5 Machi 2020
MREJELEE YESU.
Alhamisi, 27 Februari 2020
JIFUNZE KUMTUMAINI BWANA.
Jumanne, 12 Novemba 2019
USIFANYE HARAKA KUFUNGUA HUDUMA, KUHAMA KANISANI AMA KUACHA KAZI NA KUFUNGUA BIASHARA.
Na Malimu Oscar Samba:
12. Uwe na Subira, Saburi ni kitu muhimu sana, kuna wakati unakuwa katika vita vya kumiliki na kutawala lakini unakuta eneo unalotaka kumiliki au kuweka maskani yako bado hakuna nafasi, usiwe na haraka, wala usifanye haraka, endelea kuwa na uvumilivu, jambo la kuwekwa kwa adui chini ya miguu yako ni swala la mchakato, sio la siku moja, na swala la kukuwekea mazingira ya kuishi katika miliki yako kiroho iwe ni kihuduma, kiuchumi ama kiutumishi na kindoa na kadhalika linahitaji muda !
Jumatano, 30 Oktoba 2019
NGUVU YA KUWA NA UTULIVU MOYONI UNAPOKUWA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.
4. Uwe na Utulivu Nafsini Mwako, kukosa utulivu maana yake ni kuwa na mahangaiko moyoni, ni kuwa na wasiwasi au mashaka, ni hali ya kujisumbukia au kuhaha.
Hali hii ni mlango wa dhambi, maana ni adui wa imani, humuondolea mtu uwezo wa kumtegemea Bwana, maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari liwezalo kupelekwa huku na kule na upepo !
Kukosa utulivu ni kukosa raha, ni kupungukiwa kwa kiasi kikubwa na amani, ambayo hiyo amani ni njia ya Mungu kuongea, maana maandiko husema kuwa na amani ya Kristo iamuwe mioyoni mwenu, kwa hiyo hayo mazingira humzuilia Mungu kuamua ndani yako, lakini pia amani ni njia ya Mungu kukuongoza, sasa ikipotea maana yake hutaiona njia, ndio maana dalili kubwa ya mtu aliyekosa utulivu na matokeo yake ni kuwa kama mtu aliyeko njia panda asiyejua njia ya kuiendea !
Jumatatu, 14 Oktoba 2019
HISTORIA YA WOKOVU, AMA SIMULIZI ya Uamsho wa MASAMA MUDIO. Sehemu ya 6, Zamani Enzi za Askofu Imanueli Lazaro
.
![]() |
| Kulia ni Mwandishi wa Makala hii Mwalimu Oscar Samba akiwa na Msimulizi wetu Mch. Theofilo |
Tuanze simulizi yetu; Niliokoka mwaka wa 1962 January na Mungu kuniita mwaka huo huo, niliunganika na kanisa huko Mbuguni, ambako kanisa nililikuwa halijaanza huko, (la wokovu) nilipokoka tukaanza kushuhudia nyumba kwa nyumba kama vijana.
Nakumbuka kuna mama mmoja kipindi hicho alishikwa na kansa, huyu mama sikuwahi kumuona kanisani maana alikuwa mgonjwa na alikuwa amekonda sana,
Jumatano, 2 Oktoba 2019
UJUZO WA HISTORIA YA UAMSHO WA MASAMA KAMA INAVYOSIMULIWA NA Afuraeli Munisi, Sehemu ya 5.

Sikumbuki tarehe wala mwezi ila ni mwaka huo baada ya wao kuanza kushuhudia huko Arusha kidogo,hapo awali alikuwa ni mshirika wa KKT, na mama yake na baba yake pia, baba alikuwa ni mzee wa kanisa mtunza hazina wa hiyo dini, anaendelea kusimulia Mzee Munisi ! ( Ambae kwa sasa ni mzee wa miaka 83 na mke wake ni 72, aitwae Anarabi Afuraeli Munisi, ambao kwa kweli wamezeeka na mzee hapa huongea kwa utulivu maana pia sio buheri sana wa afya.)
Tunaendelea !

Walipokuja ndo walikuja
Jumamosi, 28 Septemba 2019
UWEKEZAJI WA ULIMWENGU WA ROHO KATIKA KIZAZI AU UZAO.
22 Ndipo mtakapowaarifu watoto wenu mkisema, Israeli walivuka mto huu wa Yordani, kwa njia ya nchi kavu.
Mahali: Kanisa la TAG Mudio Masama, {Jerusalem Temple} Kilimanjaro, ndilo liiloasisiwa na Askofu Lazaro na kuwa kitovu cha Uamsho maeneo mengi Tanzania:
Tarehe: 27 na 28/9/2019. Na Mwalimu Oscar Samba.
Utangulizi:
Unapoona neno uwekezaji maana yake ni kunuia kupata faida, au kuna kitu kinapandwa, au kuwekwa, chenye nia ya kuzalisha ili kumpatia mwekezaji faida.
Katika uwekezaji kuna mwekezaji, eneo, kitu kinachowekezwa/bidhaa, na soko au walaji, na alikadhalika kiroho wawekezaji ambao ni aidha Mungu au adui Shetani, wote hawa eneo lao ni duniani wakinuia kumpata mwanadamu.
Ijumaa, 27 Septemba 2019
HISTORIA YA UAMSHO WA MASAMA ENZI ZA ASKOFU LAZARO, Ikisimuliwa na Jereremia Balitomayo Kimaro, mdogo wake na mchungaji Wilson Kimaro, Sehemu ya 4.
![]() |
| Kushoto ni mwandishi wa makala hizi Oscar Samba akiwa na msimulizi wa sehemu hii ya nne Jeremia B. Kimaro wakiwa nyumbani kwake Mudio au Modia kama inavyotamkwa na wenyeji eneo la Masama. |
Anasimulia; Tulikuwa wadogo ila kumbukumbu tunayo, miaka ya 1959 na 60 ndo uwokovu ulianza, Lazaro Askofu aliupatia kutoka Arusha, na kuja na kumkuta baba yetu (Bartolome Kimaro) ambaye alikuwa ni mdhaifu au mlemavu kidogo, na baba aliukubali, Walutheri ndio waliotufanyia fujo sana.
Wengine walipigwa mfano Mzee Lazaro na Sikustaili, pamoja na Mch Robert ambae aliwahi kupigwa chuma ya kichwani kwenye paji la uso.
Fujo ilipozidi sana walikimbia, anaendelea kusimulia mzee Jeremia, anasema kuwa mmishenari aitwae Pauli Brutoni nae alikimbia na kwenda kuita polisi !
Walipokuja mimi nilimpowenti mmoja na kusema ni huyu, walimchukuwa na kumpeleka magereza, akakaa huko kama miaka miwili, na alipokuja alisema lazima atanifanyia kitu na kuja kuniua !
Alhamisi, 26 Septemba 2019
Wajuwe Mashujaa waliochochea Uamsho wa Injili au Wokovu Masama Mudio, yupo Askofu Emanueli Lazaro, pia Rev. Au Mchungaji Wilson Kimaro, Sehemu ya 3.
Eneo hili la modio Masama kipondi hicho cha mwaka 1959 kuanzia mwezi wa 12 kuna maajabu makubwa ya kiroho yalitokea, (kama sehemu zijazo zinenevyo,) na hawa ndio washirika na watendaji wa mwazoni kabisa.
1. Askofu Imanueli Kundandumi Mwasha( Askofu Lazaro.)
2. Mrs. Evagrace Imanueli.
3. Rev. Wilson B. Kimaro.
4. Firyandian Kundandumi.
5. Nkira Aranya Bartolomayo
Jumanne, 24 Septemba 2019
TUNAENDELEA NA HISTORIA NA DODOSO LA WOKOVU KIPINDI CHA ASKOFU LAZARO HUKU MUDIO MASAMA. Sehemu ya 2.
Kumbuka kuwa hili ndilo eneo ambalo ni chimbuko la wokovu kwa makanisa megi kanda ya Kaskazini na chazo cha uzalishaji wa matumishi wengi kama sehemu yetu ya tatu ishuhudiavyo kwa nchi Nzima !
Jumatatu, 23 Septemba 2019
Udodoso wa Historia na Ueneaji wa Kanisa la Tag na Wokovu kipindi cha Askofu Imanueli Lazaro Mwasha. Sehemu ya 1
NIPO MASAMA MOSHI KWA ASKOFU LAZARO NADODOSA HISTORIA YA KANISA LA TAG
Jumamosi, 21 Septemba 2019
MSAADA KWA WALIOWAI KUMWAGA DAMU YAANI KUUA:
Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu changu cha SABABU ZA DAMU YA YESU KUWA NA NGUVU ILIYO NAYO.
Kama uliwai kuua mtu, kwa kukusudia au bila kudhamiria, kwa njia ya ajli, au kutumia silaha, kutoa mimba, ukiwa kama mama wa mtoto, baba, dakitari, au kushiriki kiushauri ama kiuwezeshaji ama kwa njia yoyote ile.
Pia hata kama ulihusika katika mauaji ya mtu au watu, kwa njia yoyote, ikiwemo ya ushauri, kupanga mipango, au unafahamu fika na bayana kuwa damu ya mtu fulani ipo juu yenu, au juu yako, au katika eneo unaloishi njia hii itafanyika msaada kwako au kwenu Lakini pia hata kama wewe ni asikari, au mwanajeshi, na uliwai kumwaga damu, haijalisha uliona ina hatia au la,










