Ijumaa, 29 Desemba 2017
Jumapili, 24 Desemba 2017
Jumatano, 13 Desemba 2017
Jumanne, 12 Desemba 2017
Jumapili, 10 Desemba 2017
Jumatatu, 4 Desemba 2017
Jumapili, 12 Novemba 2017
Jumamosi, 4 Novemba 2017
HUDUMA YA MWALIMU OSCAR VITABU: NI KESHO UZINDUZI WA VITABU VYA USIFIE JANGWANI NA...
HUDUMA YA MWALIMU OSCAR VITABU: NI KESHO UZINDUZI WA VITABU VYA USIFIE JANGWANI NA...: Kava la kitabu cha ISHI SALAMA KWENYE NDOA CHANGA na MWALIMU OSCAR SAMBA wa HUDUMA ya MWALIMU OSCAR VITABU Kava la kitabu cha USFIE JA...
Jumanne, 18 Julai 2017
NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 14.
Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Ninakukaribisha ndugu msomaji wangu katika safu hii ya mafundisho ya Neno la Mungu kupitia
makala zetu, leo tunamalizia kulitazama kabila la Yuda.
Mstari unaofwata una mantiki ya aina yake katika hii
Nguvu ya Kiagano,
12 Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.
12 Macho yake yatakuwa mekundu kwa mvinyo, Na meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.
Wekundu wa macho unawakilisha Ghadhabu na Mvinyo kulevia,
weupe wa meno ni umaridadi wa maneno yake ama hotuba zake. Tukimtazama Yesu
alikuwa ni mwenye hekima kinywani mwake na aliyekubalika kwa maneno yake.
Kwa uapnde wa Mvinyo ama kulevia na Ghadhabu wasomaji wa
maandiko wanafahamu fika ya kwamba ipo silaha ya ajabu sana ya kupigania vita
kwenye ulimwengu wa roho itwayo kikombe cha ghadhabu, kikombe hiki hulevia
kisha huaribu na kuangamiza. Mimi binafsi hukitumia sana kikombe hiki
ninapokuwa nikipigana vita vya kimaagano na mizimu. Maana hutambua silaha hii
ina nguvu ya ziada katika hivyo vita.
NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 13.
Na Mwalimu Oscar Sama wa Ug Ministry.
Asante Yesu Kristo kwa majira haya mazuri
uliyonikutanisha na msomaji wangu huyu, Leo mpendwa ni sehemu ya kumi na tatu
ya makala hii na tunaendelea kuitanzama Nguvu ya Agano kwa kabila la Yuda.
Tutaanze na ule Mstari wa kumi,
10 Fimbo ya
enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata
atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.
Nisikilize, Baraka hizi zilinenwa miaka mingi ila zilibeba
hatima nzima ya kiutawala na kifalume katika Iziraeli na Ulimwengu mzima.
Fimbo maana yake ni Mamlaka, tuna fahamu kuhusu habari za
fimbo ya Haruni na Musa, kwa hiyo swala la Utawala katika Izireli lilikuwa
chini ya kabila hili, ndio maana tunamuona Mfalume Daudi, Sulemani, na wengineo
ambao walitoka katika hili kabila na kuwa watawala wenye historia kubwa.
Kisha anatajwa
Mwenye Miliki ambaye mataifa watamtii huyu sio mwingine bali ni YESU.
Hii ni Nguvu ya Agano ya ajabu sana, ya kwamba usipo ifahamu unaweza ukaona
mambo yanatokea kwenye maisha ukadhani yanakuja bahati mbaya ama kwa
kubahatisha kumbe tayari mpangilio upo.
Jambo hili halikuishia hapo bali hata Nabii Isaya alilinena
katika kulithibitisha kisha likaja jithiirisha katika Agano Jipya.
Ni Isaya 9: 6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto
mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,
NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 12.
Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Furaha ya leo iliyopo Moyoni Mwangu ni zaidi ya ile ya
Jana, yamkini nimatokeo ya kuvushwa kwako kiroho kwa maudhui ya ujumbe wa jana.
Leo ninakuletea matokeo ya baraka kwa makabila kumi na wawili ya Mzee Yakobo na
uwenda nikapata kibali cha kudodosa machache ila ninaanza na kabila la Yuda.
Tutaona siri ya Yesu kuitwa Simba wa kabila la Yuda ikiwa ni Jina la Kiagano
huku wengine wakisalia bila kulijua hilo.
Katika kuwabariki wanaye ambao ndiyo makabila ya Iziraeli
Mzee Yakobo aliwatamkia maneno ya baraka yaliyoambatana nao hadi kwenye hatima
ya Maisha yao yote.
Tuone, Mwanzo 49: 1 Yakobo
akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za
mwisho.
2 Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo, Msikilizeni Israeli, baba yenu.
2 Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo, Msikilizeni Israeli, baba yenu.
YUDA: Mwanzo 49: 8 Yuda,
ndugu zako watakusifu, Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba
yako watakuinamia.
Jambo hili limekuwa halisi, kwani Mfalume Daudi, Yesu,
Mfalume Sulemani, Ni miongoni Mwa watu waliosifiwa sana katika historia ya
Bibilia kwani wao wote ni watu wa Yuda.
NGUVU YA AGANO.Sehemu ya 11.
Na Mwalimu Oscar Samba
Ni Siku nyingine yenye fanaka tele na uzima mwingi
rohoni, ni yangu maombi kukutakia uzima huo kwa jina la Yesu kwa wewe
ulioukosa, pia udumu ndani yako kwa wewe ulio nao. Ni sehemu ya kumi na moja ya
makala yetu ya Nguvu ya Agano ikiwa ni sehemu ya kitabu changu cha NGUVU YA
AGANO KIROHO. Ninacho kibali cha kukuletea kwa njia hii ya mtandao Agano hili
moja na uwenda pia nikakudokezea lile la Yoshua lenye mizizi yake kwenye Kitabu
cha Torati ya Musa ila maagano mengine kama lile la Sinai, La Chumvi, Jipya, Daudi na hata lile la Nuhu; Huna budi
kuwa na subira hadi kitabu kitoke kisha ukinunuwe.
NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 10.
Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Laiti kungalikuwa na miwani inayoweza kukuonyesha
tabasamu nililonalo dhidi yako leo kupitia haya maandishi, ningali kuazima ama
kukununulia; Ni fika kila uchwao huwa na furaha kukupakulia chakula hiki cha
kiroho ila ya leo ina mapana yake.
Jana nilikupa ahadi ya kukuletea huu ujumbe nami sinabudi
kuitimiza hususani katika uzao wa Yusufu. Yusufu ni miongoni mwa wana wa Mzee
Yakobo aliyepitia misukosuko mingi na alishinda huku mingi ikiwa na sura ya
kiagano, tuliona alivyomiliki malango ya adui zao huko Misiri. Pia kabla ya
nduguze kuhamia ama kushuka Misiri
alikuwa amepata watoto wa wili. Manase na Efraimu.
Manase ndiye aliyekuwa wa kwanza na kisha kufwatiwa na
Efraimu; Mwanzo 41: 50 Kabla ya kuja miaka ya njaa,
Yusufu akazaliwa wana wawili, ambao Asenathi, binti Potifera, kuhani wa Oni,
alimzalia.
51 Yusufu akamwita jina lake yule aliyezaliwa kwanza, Manase, maana alisema, Mungu amenisahaulisha taabu zangu zote, na nyumba yote ya baba yangu.
52 Na wa pili akamwita jina lake Efraimu, maana alisema, Mungu amenipa uzazi katika nchi ya mateso yangu.
51 Yusufu akamwita jina lake yule aliyezaliwa kwanza, Manase, maana alisema, Mungu amenisahaulisha taabu zangu zote, na nyumba yote ya baba yangu.
52 Na wa pili akamwita jina lake Efraimu, maana alisema, Mungu amenipa uzazi katika nchi ya mateso yangu.
NGUVU YA AGANO. Sehemu ya 9.
Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Asante Yesu kwa juma pili hii njema yenye kuvutia na ya
fanaka, na pili ninakuta kimaombi kukaa na msomaji wangu huyu kwa kumsaidia
kuelewa somo hili na kulifanyia kazi. Kumbuka ndugu yangu katika Bwana wetu
YESU KRISTO leo ni siku ama ni sehemu ya tisa ya makala yetu hii na hapo jana
nilianza kukudokezea sehemu muhimu sana ya hili Agao la Ibrahimu na Mungu lililochanua
matunda kwa wana wa Iziraeli tukiwemo mimi na wewe.
Jumanne, 27 Juni 2017
NGUVU YA AGANO, Sehemu ya 8.
Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Nami sina shida kwani ni kweli waswahili husema kuwa
ahadi ni deni, nami leo sina budi kulipa deni hili, Ndugu yangu katika Kristo
kumbuka kuwa leo ni siku ya 8 ya makala yetu hii ya Nguvu ya Agano nami tokea
siku kadhaa zilizopita nalikuaidia kukuonyesha kitu muhimu ambacho Ibrahimu
alijuzwa na Mungu na hatimaye kuja kutokea kipindi cha Yakobo yaani Iziraeli
ikiwa ni Jambo la Kiagano.
Ukisoma kutoka kitabu kile cha Mwanzo sura ile ya kumi na
tano utamuona Mungu akimwambia Ibrahimu kuwa uzao wake utaenda kuishi Misiry
ama utakuwa mgeni huko na kusudi kubwa la Mungu ni kuwazidisha ama kuwaongeza,
na kuwatajirisha huko maana walitabiriwa kutoka na mali nyingi, huku muda wao
ukiwa ni miaka 400, muda ulioamariwa na Mungu, ingawaje walikaa mika 430, na
sababu za kuongezeka kwa hiyo miaka nimezielezea kwenye kitabu changu cha Namna ya Kuishi Wakati wa Majaribu au
Mapito, na pia Mungu akinipa kibali nitaligusia kwenye kitabu kile cha Wito
wa Kitumishi ili kukusaidia ujuwe umuhimu wa kumuombea Musa wako ili asichelewe
kuitika ama asikimbiliye Midiani badala yakukukomboa kwa wakati.
Tusonge mbele na Agano, Sasa leo tunaona utimiajia wa
jambo hilo ila awali ya yote ninawiwa kulidhibitisha jambo hilo ama kuliweka
bayana mbele ya macho yako.
Kwa Furaha ya Moyo Fungua nami kitabu kile cha Mwanzo
15: 13 Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya
NGUVU YA AGANO, Sehemu ya 7.
Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Ni mwingi wa furaha kwa Mungu kutuwezesha tena kukutana
siku ya leo maana sio kwa uweza wetu wala fikra zetu bali ni kwa kudra zake
Yeye liyemneemeshaji wa Neema na Baraka zote, Ameni.
Leo ni siku ya saba katika mfululizo wa hii makala yetu
ya Agano na tunaendelea kumtazama Yakobo na Uzao wake, kwa sasa tumuone Yusufu
Mwana wa Mzee Yakobo.
(k) Kupitia
Yusufu walimiliki Malango ya Misiri, Natumai unakumbuka kuwa katika
hili Agano pale Mwanzo 22 mara baada ya Ibrahimu kufaulu ule mtihani wa kumtoa
Isaka sadaka Mungu alimuaidia kummilikisha Malango ya adui zake kupitia Uzao
wake.
Tafadahali naomba tuhakiki jambo hilo ilituweze kwenda
sawia ama sanjari. Ni Mwanzo 22: 17 katika
kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za
mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa
adui zao;
Alhamisi, 22 Juni 2017
NGUVU YA AGANO . Sehemu ya 6.
Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Sifa na Utukufu ni kwa Bwana wetu Yesu Kristo, nami kwa
salamu hizo ninakukaribisha katika safu hii murwa na mubashara ya makala ambapo
leo tupo kwenye mfululizo wa 6, wa somo
letu la NGUVU YA AGANO, Ikiwa ni sehemu ya kitabu changu cha NGUVU YA AGANO
KWENYE ULIMWENGU WA ROHO.
(i) Liliamua
Mustakabali wa Maisha yao kindoa au kimahusiano, Tunafahamu
Isaka alichaguliwa mke na babaye, huku naye akimchagulia Yakobo ama
akimuelekeza mahali pakwenda kuoa, hii ikiwa na maana kwamba mwana wa Agano
haulewi na kila mtu ama haowi kila mahali kiolela.
Alikadhalika jambo hili liliendelea hadi kwa watoto wa
Yakobo yaani Iziraeli. Ukisoma katika Kitabu hiki cha Mwanzo sura ile ya 34,
utamuona binti Lea aitwaye Dina alivyochukuliwa na mtu wa ile nchi aitwaye
Shekemu mwana wa Hamori wa kabila la Hivi ama Muhivi.
NGUVU YA AGANO SEHEMU YA 5.
Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Ninakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo ndugu msomaji wa makala hii ikiwa ni sehemu ya tano, na jana nilikuaidi kuendelea na kipengele kinachoonyesha jinsi Yakobo alivyobarikiwa katika Agano hili.
(h) Kubarikiwa kimali na kurudishwa katika nchi ya Nyumbani, Kumbuka kuwa Yakobo alikuwa akiishi katika nchi isiyo yake ama ya baba zake naye alikuwa kwa Labani ama kwa mjomba ake, ila majira haya Mungu anatumia Agano hili kumtoa huko pamoja na kumpa mali.
Tutayatazama hayo maandiko lakini nataka uyaone kwa sura ya kiagano. Yaana anza kwa Yakobo kuanza mipango ya kuondoka mara baada ya Mungu kumpa kibali na hapo anaongea na wake zake, katika hayo mazungumzo kunatajwa kitu kama mimi ni Mungu wa Betheli, katika mstari wa 13.( 13 Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.)
Ninakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo ndugu msomaji wa makala hii ikiwa ni sehemu ya tano, na jana nilikuaidi kuendelea na kipengele kinachoonyesha jinsi Yakobo alivyobarikiwa katika Agano hili.
(h) Kubarikiwa kimali na kurudishwa katika nchi ya Nyumbani, Kumbuka kuwa Yakobo alikuwa akiishi katika nchi isiyo yake ama ya baba zake naye alikuwa kwa Labani ama kwa mjomba ake, ila majira haya Mungu anatumia Agano hili kumtoa huko pamoja na kumpa mali.
Tutayatazama hayo maandiko lakini nataka uyaone kwa sura ya kiagano. Yaana anza kwa Yakobo kuanza mipango ya kuondoka mara baada ya Mungu kumpa kibali na hapo anaongea na wake zake, katika hayo mazungumzo kunatajwa kitu kama mimi ni Mungu wa Betheli, katika mstari wa 13.( 13 Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.)
Jumatatu, 19 Juni 2017
RATIBA YA MIKUTANO YETU KUANZIA MWEZI WA 7 MWAKA HUU 2017 NA KUENDELEA
MWEZI WA 7, TUTAKWEPO ROMBO KWENYE VIWANJA VYA SOKO LA MAMSERA NA MANDA PALE SOKONI KILESI. MWEZI WA 8 AU WA 9 TUTAKWEPO TANGA. NA MWEZI 3 MWAKA 2018 TUTAKWEPO KWENYE VIWANJA VYA RELI HAPA MKOANI ARUSHA. BAADA YA HAPO TUTAELEKEA ZANZIBAR ENEO LA DARAJANI KWENYE KIWANJA KILICHOPO MKABALA NA DARAJANI HOTELI. KUMBUKA MIKUTANO YOTE HIYO NI YA SEMINA YA NENO LA MUNGU. ILA KATKA MWAKA HUU PIA TUTAELEKEA KARATU NA TUTAKUJUZA TAREHE.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)