Jumanne, 27 Juni 2017

NGUVU YA AGANO, Sehemu ya 8.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Nami sina shida kwani ni kweli waswahili husema kuwa ahadi ni deni, nami leo sina budi kulipa deni hili, Ndugu yangu katika Kristo kumbuka kuwa leo ni siku ya 8 ya makala yetu hii ya Nguvu ya Agano nami tokea siku kadhaa zilizopita nalikuaidia kukuonyesha kitu muhimu ambacho Ibrahimu alijuzwa na Mungu na hatimaye kuja kutokea kipindi cha Yakobo yaani Iziraeli ikiwa ni Jambo la Kiagano.

Ukisoma kutoka kitabu kile cha Mwanzo sura ile ya kumi na tano utamuona Mungu akimwambia Ibrahimu kuwa uzao wake utaenda kuishi Misiry ama utakuwa mgeni huko na kusudi kubwa la Mungu ni kuwazidisha ama kuwaongeza, na kuwatajirisha huko maana walitabiriwa kutoka na mali nyingi, huku muda wao ukiwa ni miaka 400, muda ulioamariwa na Mungu, ingawaje walikaa mika 430, na sababu za kuongezeka kwa hiyo miaka nimezielezea kwenye kitabu changu cha Namna ya Kuishi Wakati wa Majaribu au Mapito, na pia Mungu akinipa kibali nitaligusia kwenye kitabu kile cha Wito wa Kitumishi ili kukusaidia ujuwe umuhimu wa kumuombea Musa wako ili asichelewe kuitika ama asikimbiliye Midiani badala yakukukomboa kwa wakati.

Tusonge mbele na Agano, Sasa leo tunaona utimiajia wa jambo hilo ila awali ya yote ninawiwa kulidhibitisha jambo hilo ama kuliweka bayana mbele ya macho yako.

Kwa Furaha ya Moyo Fungua nami kitabu kile cha Mwanzo 15: 13 Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya

NGUVU YA AGANO, Sehemu ya 7.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Ni mwingi wa furaha kwa Mungu kutuwezesha tena kukutana siku ya leo maana sio kwa uweza wetu wala fikra zetu bali ni kwa kudra zake Yeye liyemneemeshaji wa Neema na Baraka zote, Ameni.

Leo ni siku ya saba katika mfululizo wa hii makala yetu ya Agano na tunaendelea kumtazama Yakobo na Uzao wake, kwa sasa tumuone Yusufu Mwana wa Mzee Yakobo.
(k) Kupitia Yusufu walimiliki Malango ya Misiri, Natumai unakumbuka kuwa katika hili Agano pale Mwanzo 22 mara baada ya Ibrahimu kufaulu ule mtihani wa kumtoa Isaka sadaka Mungu alimuaidia kummilikisha Malango ya adui zake kupitia Uzao wake.
Tafadahali naomba tuhakiki jambo hilo ilituweze kwenda sawia ama sanjari. Ni Mwanzo 22: 17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;

Alhamisi, 22 Juni 2017

NGUVU YA AGANO . Sehemu ya 6.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Sifa na Utukufu ni kwa Bwana wetu Yesu Kristo, nami kwa salamu hizo ninakukaribisha katika safu hii murwa na mubashara ya makala ambapo leo tupo kwenye mfululizo wa 6, wa  somo letu la NGUVU YA AGANO, Ikiwa ni sehemu ya kitabu changu cha NGUVU YA AGANO KWENYE ULIMWENGU WA ROHO.
(i) Liliamua Mustakabali wa Maisha yao kindoa au kimahusiano, Tunafahamu Isaka alichaguliwa mke na babaye, huku naye akimchagulia Yakobo ama akimuelekeza mahali pakwenda kuoa, hii ikiwa na maana kwamba mwana wa Agano haulewi na kila mtu ama haowi kila mahali kiolela.
Alikadhalika jambo hili liliendelea hadi kwa watoto wa Yakobo yaani Iziraeli. Ukisoma katika Kitabu hiki cha Mwanzo sura ile ya 34, utamuona binti Lea aitwaye Dina alivyochukuliwa na mtu wa ile nchi aitwaye Shekemu mwana wa Hamori wa kabila la Hivi ama Muhivi.

NGUVU YA AGANO SEHEMU YA 5.

Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.
Ninakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo ndugu msomaji wa makala hii ikiwa ni sehemu ya tano, na jana nilikuaidi kuendelea na kipengele kinachoonyesha jinsi Yakobo alivyobarikiwa katika Agano hili.
(h) Kubarikiwa kimali na kurudishwa katika nchi ya Nyumbani, Kumbuka kuwa Yakobo alikuwa akiishi katika nchi isiyo yake ama ya baba zake naye alikuwa kwa Labani ama kwa mjomba ake, ila majira haya Mungu anatumia Agano hili kumtoa huko pamoja na kumpa mali.
Tutayatazama hayo maandiko lakini nataka uyaone kwa sura ya kiagano. Yaana anza kwa Yakobo kuanza mipango ya kuondoka mara baada ya Mungu kumpa kibali na hapo anaongea na wake zake, katika hayo mazungumzo kunatajwa kitu kama mimi ni Mungu wa Betheli, katika mstari wa 13.( 13 Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.) 

Jumatatu, 19 Juni 2017

RATIBA YA MIKUTANO YETU KUANZIA MWEZI WA 7 MWAKA HUU 2017 NA KUENDELEA

 MWEZI WA 7, TUTAKWEPO ROMBO KWENYE VIWANJA VYA SOKO LA MAMSERA NA MANDA PALE SOKONI KILESI. MWEZI WA 8 AU WA 9 TUTAKWEPO TANGA. NA MWEZI 3 MWAKA 2018 TUTAKWEPO KWENYE VIWANJA VYA RELI HAPA MKOANI ARUSHA. BAADA YA HAPO TUTAELEKEA ZANZIBAR ENEO LA DARAJANI KWENYE KIWANJA KILICHOPO MKABALA NA DARAJANI HOTELI. KUMBUKA MIKUTANO YOTE HIYO NI YA SEMINA YA NENO LA MUNGU. ILA KATKA MWAKA HUU PIA TUTAELEKEA KARATU NA TUTAKUJUZA TAREHE.

Mwalimu Oscar Samba: MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA.

Na Mwandishi wetu, Ug Ministry.

Hakika kwetu Jehova Jire ni Ebeneza maana sio kwa uweza wetu bali ni kwa nguvu zake ndiposa tunayanena hayo. Jana tulifanikiwa kuhitimisha semina yetu huku nguvu za Mungu zikishuka mahali pale, watu wakifunguliwa na hakika semina ilikuwa ya Baraka maana licha ya watu kunufaika na mafundisho pia wapo waliookoka.

Kama ilivyo ada Mwalimu jana alianza kwa kuwaimiza wakristo kumtafuta Mungu kwanza na haki yake kisha hayo mengine yote wanayoyahitaji kutoka kwake Yeye atawajaza.

Siku ya jana Mwalimu alihitimisha kwa Mbinu ya 9, nayo ni ; Kufahamu athari za kuwa na Mali isiyo na Yesu. Katika hili alisisitiza mathara yanayoweza kujitokeza kwa mtu mwenye mali kisha akamkosa Yesu kwenye Uchumi wake.
Alinza na andiko lile la Ufunuo wa Yohana 3: 17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

Mwalimu Oscar Samba, Mbinu Teule za Kutoka Kwenye Umasikini Kwa Watu Wal...

Jumapili, 18 Juni 2017

PICHA ZA SEMINA YA NENO LA MUNGU SIKU YA 8, MOROMBO ARUSHA TANZANIA; Na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry, Somo: MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA.






Mwalimu Oscar Samba: MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA.

Mwalimu Oscar Samba
 Na Mwandishi wetu, wa Ug Ministry.

Ninakukaribisha sanjari na kukusalimu kwa jina lake Bwana wetu Yesu Kristo aliye pia Mwokozi wetu.Leo ni siku ya saba ya Semina Yetu na kumbuka somo hili ni la jana kwa hiyo kijografia jumapili ya leo ndiyo tunahitimisha semina hii ikiwa ni siku ya nane na ujumbe wa nane utaupata kesho.

Mwalimu jana alitilia tena msisitizo wa kukutaka kuutafuta kwanza Ufalume wake Yesu Kristo na Haki yake kisha hayo mengine utazidishiwa. Pia jana alifundisha mbinu moja kuu ambayo ilikuwa ni mbinu ya Akili, Hekima na Maarifa. Mwalimu alivifafanua vitu hivyo kwa mapana na kukuhitaji kuhakikisha ya kwamba una vifahamu ili uweze kunufaika na vitu hivyo.

Alitoa mfano wa Mfalume Sulemani aliyeomba hivyo vitu, 1 Wafalume 3:4-15, ila alisoma mstari wa12 na kukutaka mingine kujisomea.
12 basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.

Mwalimu Oscar Samba, Mbinu Teule za Kutoka Kwenye Umasikini Kwa Watu Wal...

Jumamosi, 17 Juni 2017

Picha za Semina ya Neno la Mungu Kutoka Morombo Arusha Tanzania na Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry, Somo: MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA, 7.

Mwalimu Oscar Samba


Mchungaji Denisi akifungua kwa Maombi.

Mwalimu Oscar Samba: MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA 6.

Na Mwandishi wetu wa Ug Ministry.
Ninakukaribsha katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi wa maisha yetu katika safu hii ya ujumbe wa Semina ya Neno la Mungu ikiwa ni siku ya sita kama ilivyofundishwa jana na Mwalimu.

Mwalimu alianza kwa msisitizo kwamba ili kufanikiwa Kiroho na kiuchumi ama kufikia mafanikiao ya kutajirika kiuchumi katika Kristo Yesu yatupasa kuutafuta kwanza Ufalume wa Mbinguni na Haki yake na kisha hayo tunayaoyahitaji tutayapata.

Jana alifundisha mbinu moja nayo ilikuwa ni KULIJUA KUSUDI LA MUNGU LA KUKUTAJIRISHA, katika mbinu hii Mwalimu aliwataka walio matajiri kufahamu jambo hili na kuliishi huku akiwafundisha wale wenye nia au kiu ya kutajirika kupitia mfumo wa kimbingu kuhakikisha wanalifahamu na kuliisha kusudi hili ili Mungu awatajirishe na akisha kuwatajirisha wahakikishe wanalitimiza hili kusudi ili mali ama fedha zisiwatowe kwake.

PICHA ZA SEMINA YA NENO LA MUNGU SIKU YA 6, MOROMBO ARUSHA TANZANIA NA MWALIMU OSCAR SAMBA KATIKA SOMO LA MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA 6.

Kushoto ni Mwinjilisti na Mwalimu SixMon akiwa na Mwalimu Oscar Samba katika Mkutano huo wa Semina


Mwalimu Oscar Samba, Mbinu Teule za Kutoka Kwenye Umasikini Kwa Watu Wal...

Ijumaa, 16 Juni 2017

Mwalimu Oscar Samba, MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA, 5.

Mwalimu Oscar Samba akifundisha katika semina
 jana hapa Morombo Arusha Tanzania
Na Mwandishi wetu, Ug Ministry.
Ninakukaribisha katika jina la Yesu Kristo Bwana wetu na Mwokozi wetu katika sehemu hii ya 5 ya ujumbe wetu kama alivyofundisha Mwalimu jana kwenye semina inayofanyika hapa mkoani Arusha kwenye viwanja ya Morombo nchini Tanzania.

Kama ilivyo ada alianza kwa kutoa msisitizo kwa watu kuutafuta kwanza ufalume wa mbinguni na haki yake na kisha hayo mengine ikiwemo ya uchumi ama utumishi watazidishiwa.

Mwalimu wetu alitoa utangulizi uliyolenga kuwakumbusha wanafunzi wake mahali aliponzia tangu siku ya kwanza na kusema ya kwamba alitamani kugusia somo la Agano la Chumvi ili kuwasaidia watumishi wa Mungu maana ni Agano la kitumishi ila kwa jana hakupata kibali ila siku ya mwisho ya semina huenda akakipata na ikumbukwe kuwa hasemi jambo kwa akili zake bali hunena lile ambalo Roho anataka alinene kwa wakati gani na sehemu gani.

Mwalimu Oscar Samba, Mbinu Teule za Kutoka Kwenye Umasikini Kwa Watu Wal...

Alhamisi, 15 Juni 2017

Picha Za SEMINA YA NENO LA MUNGU, MOROMBO ARUSHA TANZANIA SIKU YA 5, NA Mwalimu Oscar Samba wa Ug Ministry.



Mwalimu Oscar Samba, Mbinu Teule za Kutoka Kwenye Umasikini Kwa Watu Wal...

Mwalimu Oscar Samba: MBINU TEULE ZA KUTOKA KWENYE UMASIKINI KWA WATU WALIOOKOKA.

Mwalimu Oscar Samba
 Na Mwandishi wetu, Ug Ministry.

Ninayo furaha murwa kabisa nami bila iyana wala hofu ninakukaribisha katika sehemu ya nne ya ujumbe wa semina yetu mubashara inayoendelea hapa mkoani Arusha nchini Tanzania kwenye viwanja vya sokoni Morombo.

Jana Mwalimu alianza kwa ufafanuzi wa somo ambalo tunaendelea nalo wiki hii yote na katika hilo alichambua kiundani andiko la msingi ama la semina linalotutaka kuutafuta kwanza ufalume wa Mbinguni na haki yake na kisha hayo mengine yote tutazidishiwa. Alisema ni vyema kumtafuta Mungu kwanza kisha katika hapo ndipo tutapata Hekima, Akili na Moyo wa Maarifa; vitu ambavyo vitatusaidia kufanikiwa kiuchumi.

Alitanabaisha kuwa, hakuna mtu anayetaka kuwa dakitari kwa kuanza na kozi ya udakitari ama kushika sindano na kuvaa joho jeupe kisha kuanza kujiita ama kutaka kuitwa dakitari.