KURASA

Alhamisi, 26 Machi 2026

Aina za Upako

Pichani ni Mwl. Oscar Samba, akiwa anatoka Shambani akijikinga mvua kwa njia ya Asili: anatumia jani la gimbi kujifunika.
 Huku ikisadifu maudhi haya kwa kutuonyesha alipokuwa anapitia. Ambapo utapaelewa katika kitabu chake cha IMANI INAPOJARIBIWA na Kile cha KWA NINI MUNGU ANATUTAKA TUSIJILIPIZIE KISASI?.

 #AINA ZA #UPAKO

1. Upako Unaotokana na Mahali Unapopitia

2. Upako Unaotokana na Maombi

3. Upako Unaotokana na Neema au Karama. Au Unao ambatana na Wito ama Mafuta. (Ingawa kuna ambaye ana Mafuta ya Wito 'kila aliyeitwa hupewa.' Na kuna yule mwenye mafua hayo pamoja na neema ya ziada ambapo huitwa Karama.

4. Upako Unaotokana na Utii wako kwa Mungu katika Maelekezo aliyokupatia. Mfano aina ya ujumbe, kibali cha kuhudumu eneo au mahali husika na kadhalika. (Mapenzi Makamilifu ya Mungu.)

5. Upako Unaotokana na Kuombewa, au Kubandikwa Mikono na Muhubiri au mtumishi fulani. Paulo anamueleza Timotheo ya kwamba kuna aina ya mafuta aliyapata kwa kuwekewa mikono na wazee. (Uwe makini sio kila mzee amebeba roho sahihi.) 

Aina Nyingine

 6.Tukio Maalumu la Kutembelewa na Nguvu za Mungu Katika Ibada. 

7. Uwezo wa Kufuata Maelekezo Maalumu Yanayokuja Saa hiyo hiyo Unapokuwa Madhabahuni.

Huambatana na matumizi ya karama nyingine kama za neno la maarifa, unabii, kupambanua roho na kadhalika.

8. Upako Unaotokana na Neno la Mungu Lenye Uzima. (Waliokuwa wanashangaa mafundisho ya Yesu ya kuwa alikuwa akifundisha tofauti na waandishi wao; kuna kitu cha namna hii walikutana nacho. (Kitabu chetu cha UTUMISHI WENYE MATUNDA MBELE ZA MUNGU; kitakusaidia kulielewa hili zaidi.

9. Upako Unaotokana au Uliopo Ndani ya Mafunuo. Waefeso huutaja kama roho ya mafunuo na hekima. Ni watumishi wachache wanaoijua hii siri.

10. Upako Unaotokana na Imani ya Anayeombewa. Matendo ya Mitume 14:9 Mtu huyo alimsikia Paulo alipokuwa akinena; ambaye akamkazia macho na kuona ya kuwa ana imani ya kuponywa.

Utamuelewa Yesu sasa ni kwa nini alikuwa akimjengea mtu imani kwanza ya uponyaji kabla ya kumuombea. Ni ili akutanishe imani yake na ya Yesu. Katika Yohana 11 anahakikisha Matha amejaa imani ya ufufuo ili amfufue kwanza Lazaro. 

Hapa watumishi wengi wa ukanda wa Afrika Mashariki tunakwama. Tunaona ni kushuka kiroho kumjengea muhusika imani kwanza. Ndio maana eneo la matendo ya miujiza hatuna matokeo makubwa sana kama wenzetu wa ukanda wa Kati na Afrika ya Magharibi.

Yule mtu aliyemwambia Yesu nisaidie kwa kutokuamini kwangu ni mfano mzuri sana. (Usilazimishe imani yako kama muhubiri au mtumishi pekee ifanye maajabu.

 Hatukuumbiwa hili kila wakati. Jifunze kanuni hii na itakusaidia. Mungu aliiweka ili kuhakikisha muhusika naye anakuwa sehemu ya muujiza huo ili kumuondolea kukuabudu. Badala yake awe na msingi wa kuweka imani kwa Yesu.

Wahubiri wengi wa imani potofu hili hawalifanyi. Na wa imani sahihi hili nalo hawalijui. Lakini tazama miujiza mingi ya Yesu utakutana na imani shirikishi. Yaani imani ya Baltomayo kipofu na Yesu. Kitendo cha Yesu kumuuliza wataka nikufanyie nini? Kinatosha kutupa kutambua ya kuwa kuna namna Yesu alihitaji kukutanisha zile imani mbili.

Kwa mujibu wa Waebrania 11:1, imani imebeba dhima ya kuwa na tarajio. Baltomayo kipofu alitarajia kuona. Ndio sababu ya Yesu kumuuliza nikutendee nini? Wengine aliwauliza je, wataka kuwa mzima?

Mama aliyetokwa na damu miaka 12 yule wa Marko 5, Yesu anamwambia ya kuwa, mama imani yako imekuponya na usiwe na msiba wako tena!

Umeona kitu hapo! Sio imani yangu Yesu imekuponya, bali ni imani ya yule mama!

Sasa, mimi na wewe tunataka imani zetu kama waombeaji zitende kazi tu! Hii huwa mara chache-chache sana. 

11. Upako Unaotokana na Uwepo wa Mungu Juu/ Katika Kusanyiko la Mahali Pamoja, Dini yaani Dhehebu au Taasisi. Yaweza kuwa pia familia kama kusanyiko la kiibada, kikundi cha maombi, kwaya au timu ya kusifu wa na kuabudu.

Musa akamwambia Mungu, uwepo wako usipoenda pamoja nasi usituchukue mahali hapa. (Kutoka 33:15 Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa.  And he said unto him, If thy #presence  go not with me, carry us not up hence.)

Namna ya Kuutunza....

Sababu Zinazoweza Kuupoteza...

Namna ya Kuurejesha.

Dalili Zitakazokujulisha kuwa Upo au Haupo.

1. Umwagiko wa Nguvu za Roho Mtakatifu katika Kusanyiko Husika. (Zaidi ni Kwenye Kitabu Chake..)

12. Upako Unakaa au Uliopo Katika Eneo, Aridhi, Anga, Nyumba, Chombo cha Usafiri,  ama Madhabahu (kama eneo maalumu la kiibada.) Hata ule upako unakaa kwenye vitu kama vitabu, maandiko ama machapisho fulani fulani ya kiroho, mtandaoni: kama kwenye blogu au tovuti na kurasa mbalimbali; huingia katika hili kundi.

Mfano kwa Musa, alipoambiwa avue viatu aridhi ile ni takatifu, kuna namna ilimanisha katika eneo lile, kuna uwepo wa nguvu za Mungu kipekee. (Katika aridhi.)

Unapomsikia mtu anasema anga la mahali hapa ni gumu, kuna namna uwepo wa nguvu za Mungu ni mchache ukilinganisha na ule wa adui. Ama kuna namna adui anamiliki hilo anga, (uwepo wake angani.)

Mfano wa Yakobo, katika Mwanzo 28, analipoona ngazi ikiwa na urefu kutoka aridhini hadi mbinguni, akasema mahali pale Mungu yupo.

Namna ya Kutengeneza Mazingira ya Upako Huu Kukaa Katika Eneo Lako. Iwe la Kiibada au kibiashara na hata Kimakazi.

(Utaikuta Kwenye Kitabu Chake..)

13. Upako Unaokuja Mara Baada ya Mtu Kukubali Kuokoka au Anapofanyika Kuwa Mwana. Kumbuka upako maana yake ni nguvu za Mungu. (Alitupa uweza wa kufanyika wana wa Mungu, Ambao Ndio Sisi Tuliaminio Jina Lake. Yohana ....) Uweza maana yake upako. Na uweza katika Biblia una tafsiri ya nguvu za Mungu zilizogeuka kuwa utendaji. Ama ni nguvu katika uwezeshaji. Kinachomuokoa mtu ni nguvu za Mungu, ambazo hufanya kazi katika kumuokoka yaani kumuhamisha kutoka katika uflme wa Shetani, nikimaanisha wa nguvu za giza; na kisha kumuingiza katika ufalme wa Yesu. Ni Wakolosai.... Na wakati huo huo, tukifanywa kuwa wana wa Mungu. Haiishi hapo tu, bali hutuwezesha kuacha dhambi. Kwa kutuondolea utu wa kale, yaani matendo ya mwili. Hutupa utu mpya wa Kiungu. Hutubadilisha tabia. Faida au Utendaji wa Upako Huu. 1. Kutuokoa Kutoka Dhambini. 2. Kutuvua Utu wa Kale. 3. Kutufanya Kuwa Wana. 4. Kutupa Utakatifu/Kutuumbia . Hutuingiza Katika Agano Jipya. . Hutufanya Kuwa Warithi Pamoja na Kristo Yesu. .... Upako huu pia hufanyika kuwa ulinzi,..... NB: Ukiacha wokovu au ukikoma kuwa mwana kuna kitu cha namna hii unapoteza.(Ili kunufaika nao, kuokoka ni muhimu. Nje ya hapo nguvu ya kushinda dhambi hutakuwa nayo. Katika huu upamo ndimo mlimo na aina ya mafuta yanayokufundisha mambo mema, na mabaya. Tazama; Tito 2:11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; 12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa. Unganisha Na:1 Yohana 2:20 Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote. 27 Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.) Zaidi Kitafute Kitabu...na uchambuzi wa pointi tajwa hapa...Kikitoka kitabu kitafute Written by Mwalimu Oscar Samba 

+255759859287 Mwanza Tanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni