Jumamosi, 29 Juni 2019

MNGOJE BWANA KAMA MKULIMA ANGOJAVYO MAVUNO


Na Mwalimu Oscar Samba:
Kwenye pwenti ya kumngoja Bwana kwa Saburi; Mpendwa Mwenzangu katika Bwana ! Mwenye kungoja kwa Saburi huwa na taraja, ndani yake mna imani dhabiti, hana mashaka wala manongono, ni kama vile mkulima angojavyo mazao !
     📜Hana haraka, ana hakika yaja majira ya mavuno, kwanza hulikwatua ama huliandaa shamba hata kabla ya mvua kunyesha, hutia mbegu chini majira ya mvua ya kupandia, wakati wa palizi hana haraka ya kuvuna bali hufanya palizi, huwekea mbolea na kuyalinda dhidi ya wadudu, kisha huja wakati wa kuchanua, napo hana haraka, anajua kuna majira ya ngano au suke, ama mahindi yake kukomaa; Marko 4:26 Akasema, Ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi;

27 akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikamea na kukua, asivyojua yeye.
28 Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke.
29 Hata matunda yakiiva, mara atapeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika.
Aina hii ya uvumilivu, ndio tunaotakiwa kuwa nao, ili kutuwezesha kuyafikilia mema yetu, mwisho wa maandiko nikupayo kuna onyo kuhusu manongono ! Hii ikupe kuwa makini na mwenendo huu, wenye ishara ya kukosa au kupungukiwa saburi, (Zakaria alimngoja Bwana kweli, ila kuna namna Saburi ilipungua ! Ni kweli ilikwepo

Alhamisi, 13 Juni 2019

Muongozo wa Maombi ya Kuombea aridhi

Ni ujumbe niliomtumia mtu kama "sms"

Mngoje Bwana


Mngoje Bwana, Jipe moyo, Usife Moyo
"Yeye aliyeahidi ni mwaminifu", kwa hiyo; hiyo ni sababu moja kubwa muhimu sana inayokupasa kumngoja !
Unajua mwanadamu haaminiki kwa asilimia zote, huweza kukwambia ningoje hapa, nisubirie hapa, na kisha asije kutokea, au akakwambia nilikwama, nilipitiwa, ila sio Mungu wetu, huyu Mungu ni mwaminifu, ni wa dhati na kweli.

Kuna heri, au ipo baraka kwa wanaomngoja Bwana ! Mithali 8:34 Ana heri mtu yule anisikilizaye, Akisubiri sikuzote malangoni pangu, Akingoja penye vizingiti vya milango yangu.
Hasemi siku moja, mbili, au tatu ! Hasemi mwezi mmoja, wala miaka miwili, bali husema siku zote !

Hili ni jibu kwa wenye swali la ningoje hadi lini ? Na kufuatiwa na maelezo kama kungoja kwa kweli nimengoja sana, nimesubiri sana, ila sijibiwi ! Ni hadi haki yako ichomoze kama mwangaza, na kufanywa sifa, na unapaswa kufanya hivyo siku zote, na ungoje kwenye vizingiti vya milango yake !

Jifunze Kuongeza au Ombea Imani yako ya Kupokelea Majibu

Aina za Imani katika Kuomba, na Mwalimu Oscar Samba
 ( Unapohisi imepungua, au itapungua, ingia kwenye maombi maalumu, ) awali ya yote nikufunze kuhusi imani ya kuomba, au aina ya imani ambayo hukusukuma au hukuwezesha kufanya maombi; Marko 11:23 Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.
Wakati unaomba, unatakiwa kutokuwa na shaka, na uamini kile unachokihitaji, au kukiamrisha kiwe, kitakuwa, ama itakuwa kama vile ulivyokusudia au kunuia moyoni mwako. Ukisema ugonjwa huu toka, pona, uwe na hakika unachokihitaji kitakuwa, na ugonjwa utatoka. ( Hii ni imani inayotumika muda wa kuomba.)

Sasa ukishaomba, inakuja imani au inatakiwa iwepo imani ya kupokelea majibu, nikiwa na maana kwamba yale uyaombayo, au uliyokwisha kuyaomba, unatakiwa kuamini kuwa yamekwisha kuwa yako, pia imani hii itakusaidia kuendelea kushikilia wingu la maombi, na kukusaidia mara kwa mara kurejea katika imani ya kuomba, na kukuwezesha kuomba bila kukoma, ikiwa ni sehemu ya uhusiano uliopo kati ya aina ya kwanza na ya pili, na fahamu ya pili haiwezi kuja bila ya kwanza kufanya kazi yake.

Na sababu kubwa

Jumatatu, 10 Juni 2019

Upako ni Kulipa Gharama

Nimeandika hivi, katika kitabu chetu cha NGUVU YA KUOMBA BILA KUKOMA !
Najifunza kitu kisichochepesi kwa Elisha ! Natumai unajiuliza ni kipi tena hicho Mwalimu ! Ni hiki ! Elisha alikuwa na msimamo sana, maana Elia licha ya kumpa upinzani mzito ili kuuhakikisha moyo wake kama kweli umekusudia, kuna mthihani mwingine alimpa mara baada ya kuomba ombi lile !
2 Wafalme 2:10 Akasema, Umeomba neno gumu; lakini, ukiniona nitakapoondolewa kwako, utalipata; la hukuniona, hulipati.
Ni baada ya kuomba upako mara dufu, sasa Elia anampa shariti, kuwa akimuona saa anaondoka, atapokea, la hakumuona, hatapokea !
Huu ulikuwa ni mtihani muhimu sana, na kwa

Endelea Kumkumbusha Mungu, Kamwe Usiwe Kimya, Kaza Kuomba Bila Kukoma !

Kukaa kwako kimya kutamfanya Mungu nae kunyamaza, ila kuendelea kumzongazonga kwa maombi yako na sadaka ndiko kutakakomfanya kutokutulia, na kisha kukupatia majibu yako upesi !

Amejiaidia mwenye hapa ! Isaya 62:1 Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo.
:2 Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana.

Daudi anatuambia kuwa katika taabu yake alimlilia Bwana, kisha naye akasikia kilio chake ! Sijui wewe katika taabu yako huwa unafanyaje ?

Alhamisi, 6 Juni 2019

Muhesabu Mungu kuwa ni Mwaminifu, ni katika kitabu cha NGUVU YA KUOMBA BILA KUKOMA.

Muhesabu Mungu kuwa ni Mwaminifu, ni katika kitabu cha NGUVU YA KUOMBA BILA KUKOMA.
Kwa hiyo, Mungu akikuaidia ni hakika atalifanya hilo kuwa jema, jambo muhimu kwako ni kumuhesabu kuwa ni mwaminifu, ukijuwa vyema kazi aliyoianza ni lazima ataimaliza tu ! Wafilipi 1:6 Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu.Kama amekupa mke au mume, uwe na hakika na mwana atakupa ! Kama ameweza kukupatia biashara, uwe na hakika na swala la wateja atalimaliza. Kama ameweza kukuleta ulimwenguni, basi na uponyaji ni haki yako.

Yamkini umeliombea jambo hilo kwa muda sasa, na imefika mahali limegeuka na kuwa jaribu ! Nikimaanisha sio hitaji la kawaida, maana limeanza kukuweka njia panda na kukufanya uanze kufikiri kwa upya kuhusu uhusiano wako na Mungu, au kuhusu uendelee kumngoja Bwana kwa saburi au umngoje katika hali ambayo akitenda sawa na asipotenda pia ni sawa, ili mradi wewe unachojua ukitwaliwa leo ni mbinguni mengine hutaki tena kuyajua !

Jumanne, 4 Juni 2019

Yajuwe Majina ya Mungu na Maana Zake, mfano Adonai maana yake ni Mungu mwenye Enzi, Mwanzo 15:2-3, Eli-Shadai ni Mungu Utoshalezae, Mungu Mwenyezi, Eli-Gibo, ni Mungu Mwenye Nguvu


Usiogope Adui MTAZAME MUNGU, NA TENDA KWA AKILI . Na Mwalimu Oscar Samba.


Zaburi 56:4
Aliinuka Sauli mfalme enzi za Biblia na kujaribu kupigana na shauri la Bwana akimuwinda Daudi aliyekuwa mfalme mtarajiwa kila kona lakini mwisho wake alijikuta akiishilia kwa mganga wa kienyeji na hatimae shauri la Bwana kushinda ndani ya Daudi !
Yamkini huyo anayepigana nawe hana hata cheo cha ubalozi wa nyumba kumi, na uwenda hakuwahi kuwa hata kiranja alipokuwa shule !

Sasa kwa nini uogope ! Ni kwa nini ukubali kutishwa na mwenye mwili wakati yupo awezae kuuzima kwa dakika ama sekunde moja na hata nusu sekunde !

Enzi za wakina Petro ama kanisa la kwanza aliinuka mtu mkoja aliyeitwa Herode, na kujipiga kifua mbele za Mungu wetu ila mwisho wake aliishilia kutafunwa na mdudu hadi kufa !
Farao alijifanya kupigana na taifa teule na mwisho wak

Jumatatu, 3 Juni 2019

Mtumaini Bwana Bila Wasiwasi !

Zaburi 26:1.
Na Mwalimu Oscar Samba.       Najua kuna mambo mengi kadha wa kadha umeyaombea ila bado hujaona majibu yake ! Yangu rai ni kukusihi kuwa Bwana yu malangoni, na ana heri yule amngojae hapo, ikiwa na maana kuwa amebarikiwa aliyeweka tumaini lake kwa Bwana.

Ni muhimu sana kufahamu sana kuwa imetupasa kumuomba Mungu bila kukata tamaa, hii iwe ndio dira yetu peke maana Mungu hujibu kwa wakati wake, na inatupasa kumuomba siku zote bila kuvunjika moyo, maana sisi wenye kumkumbusha Bwana twaambiwa tusiwe na kimya, anasema ameweka walinzi juu ya kuta zako, ambao hawatanyamaza usiku wala mchana , walinzi mpendwa ni aina ya waombaji !

Kwa hiyo Bwana amekusimamishia watu

Jumapili, 2 Juni 2019

HAWA NI WATU WALIOMDHIHAKI MUNGU NA KUPATWA NA SHIDA


1. JOHN LENNON (MUIMBAJI)
Wakati alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la American alinukuliwa akisema hivi "Ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwasi na hilo kwa kuwa nina uhakika nalo. Mafundisho ya Yesu yalikuwa sahihi na wala sipingi hilo ila mafundisho yale yalikuwa mepesi sana ambayo mtu yeyote anaweza kuyafundisha. Hebu angalia leo, tumekuwa maarufu hata zaidi yake (Hapo alilitaja kundi lake la The Bettle). Ilikuwa mwaka 1966. Wiki moja baada ya kutamba kwamba yeye na kundi lake lilikuwa maarufu hata zaidi ya Yesu, akapigwa risasi sita na kufariki.
2. TANCREDO NEVES (RAIS WA BRAZIL)

Jumatano, 29 Mei 2019

Usifadhaike, Mungu anajua Unayohotaji.


Mathayo 6:8.
Nami nakuhakikishia kuwa ni Kweli na dhairi kuwa Mungu anajua unayoyahitaji, kwa hiyo huna sababu ya kufadhaika, kukata tamaa, kuhuzunika wala kujawa na wasiwasi, maana Mungu anajua unayoyahitaji, usijisumbukie, wala kupoteza muda mwingi kwa kuwazia adha uliyo nayo, Mungu anajua unayoyahitaji, hii ndio kauli yangu na ya dhati itokayo moyoni mwa Mungu wangu, maana andiko hilo, la dhibitisha hili !
Huna sababu ya kukosa usingizi, kushindwa kula, wala kukosa amani kisa una ukata, au ukwasi

Jumanne, 28 Mei 2019

WAPOLE WATAIRITHI NCHI.( Upole, Unyenyekevu kama Silaha ya Kivita.)

Na Mwalimu Oscar Samba


 WAPOLE WATAIRITHI NCHI.( Upole, Unyenyekevu kama Silaha ya Kivita.)
Ijumbe huu utaupata katika kitabu chetu cha #TEKATAWALANAUMILIKI
. Fahamu: Wapole Watairithi Nchi; Upole ama Unyenyekevu ni miongoni mwa silaha muhimu sana ya kivita, (fahamu sana kuwa upole unaotajwa kwenye maandiko sio wenye maana ya ule unaokuwa rathi kupokonywa haki yako, au kukosa ujasiri wa kujitetea, ama uzubaifu, la ! Ni upole kama tunda la Roho au kama tabia ya Rohoni, maana hata Yesu aliwahi kupinduapindua meza, kuvuruga gulio pale hekaluni akiitetea kweli ya Mungu, lakini bado alikuwa mpole, aliwahi pia kuwaambia nendeni kamwambie yule mbweha, akimlenga Herode aliyekuwa mtawala, pia aliwahi kumkaripia Petro vikali akimwambia rudi nyuma yangu Shetani, na kadhalika ila bado alikuwa mpole, twajifunza pia kwa Musa, alikuwa mpole lakini ifikapo swala la uhusiano na Mungu wake kuna namna upole ule haukuwa kikwazo maana ulikuwa ni tunda la Roho na sio hulika ya kawaida ya kibinadamu, au ule upole ambao ni matokeo ya "slow mindi" ama ufahamu uliopumbazika.
Mathayo 5:5

Alhamisi, 2 Mei 2019

SI MAPENZI YA MUNGU TUWE MASIKINI Na Mwalimu CHRISTOPHER MWAKASEGE


Utangulizi: (Namna ya mkristo kuishi katika hali ngumu ya uchumi bila kumkosea Mungu).
      Kati ya mambo yaliyotabiriwa kutokea katika siku hizi za mwisho ni dhiki katika mataifa, pamoja na hali ngumu ya uchumi. Soma mwenyewe katika Luka 21:25-26 na Ufunuo wa Yohana 6:5-6.

Pia, tunasoma kutoka katika biblia ya kuwa biashara na uweza wa kuuza na kununua utafuata mfumo fulani uliojaa dhuluma, ambao utatawaliwa na kundi fulani ulimwenguni. Watu hawatauza wala kununua bila ya kupatana na watu wa kundi hilo, na hasa kiongozi wao. Na asomaye na afahamu. Soma kitabu cha Ufunuo wa Yohana sura yote ya 13.
Si hivyo tu, bali biblia inaeleza wazi kabisa kuwa katika siku hizi za mwisho kutakuwa na uhusiano mkubwa sana kati ya utajiri na uasherati na pia kati ya biashara na uasherati. Soma kitabu cha Ufunuo wa Yohana sura za 17 na 18. Lakini pia unaweza kuwa na utajiri na ukafanya biashara bila kujihusisha na uasherati na mambo mengine yaliyo kinyume na maadili ya Mungu.

Muimbaji Faustin Munishi na Kilio cha Kushuka kwa au Kupoa kwa Moto wa Uinjilisti leo

Pichani NI MAKAMANDA WA YESU WALIOITIKISA TZ KWA INJILI.
  Ev Daudi Kuselya | Ev Emmanuel Lazaro | Ev Moses Kulola.

Ameyaeleza katika Mtandao wake wa kijamii wa Face book, unishi Muimbaji ameyasema haya ambayo kwangu leo ni changamoto, "NAKUMBUKA TULIKUWA DODOMA MWAKA 1982 KWENYE MKUTANO WA INJILI KANISA LA TAG LILILOKUWA LINAONGOZWA NA MCHUNGAJI MHINA

KABLA YA MKUTANO JIONI, NILIMWOMBA ASKOFU MOSES KULOLA WAKATI HUO MWINJILISTI WA TAIFA TAG TWENDE STUDIO TUCHUKULIWE PICHA HII.

Kushoto ni Mimi Mtumishi Faustin Munishi, Katikati ni Askofu Moses Kulola na kulia ni Aliyekuwa msaidizi wa Mwinjilisti Kulola wakati huo Mwinjilisti Emmanuel Mwasota Ambaye sasa ana Kanisa Dar.

Tulikuwa na ratiba iliyojaa kuzunguka Tanzania yote tukihubiri Injili.

Jumamosi, 27 Aprili 2019

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA.

Mahali: TAG Ushiri Rombo: Tarehe 28:2:2019. Na Mwalimu Oscar Samba.
Aliyeshika kipaza sauti (kushoto) ni mama mchungaji wa kania hili jia ni Paumelina B. Senkondo, na wengineo ni wanawake wakiimba shairi.

Mwalimu Oscar Samba

Washirika

Mwanzo 2:18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
Mwanamke ni msaidizi, andiko hilo lipo kabla ya dhambi kuingia ulimwenguni, hakukuwa na mfumo wa kanisa ama kuabudu kama leo, au kama baada ya dhambi, kusudio la ndoa, au familia ni ili liwe kanisa, yaani tuliumbwa kwa ajili ya ibada !
Kwa hiyo, kanisa, lina mukutadha wa ndoa, kwa hiyo, dhima ya mwanamke kindoa au kifamilia, ina mashabihiano na ile ya kikanisa !

Waefeso 5:23 Kwa maana

Jipatie maandiko mbali mbali ya Biblia kuhusu Damu ya Yesu, Shukurani, Ahadi za Mungu na kadhalika




KUNA MTU MMOJA MWENYE KESI AMENIOMBA NIMFUNZE NAMNA YA KUOMBA, NAMI NAKUMEGEA:

1. Omba Rehema, tubu bila kujihesabia haki, tumia Danieli 9, pia Warumi 3:25 ukiitaka Damu ya Yesu ifanye rehema, na Mathayo 26:28 kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.

2. Ifute hiyo Kesi kwa Damu ya Yesu, Waebr 9:22, futa hizo nakala/kopy za kesi ama mashitaka.

3. Gongomelea hzo hati za Mashitaka Msalabani, Wakolosai 2:14 akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;

Upole wako na ujulikane na kila mtu !

Bwana Yesu asifiwe,
Kuna Mtu aliniambia niseme Neno, nami nilisema ! Sasa nakumegea nilichomfunza !

    Upole ni Tunda la Roho, ambalo linadhima ya unyenyekevu ndani yake.

  Kazi na faida moja wapo ya upole ni kukupa majibu ya busara hata katika nyakati ngumu, haijalishi ni zenye kuuthi au kujeruhi, utajifunza kwa Yesu, na Yeremia pia, ila ona hapa;Mithali 15:1 Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.

Upole unakuwezesha kuepukana na mitego ya adui, inauonuia kukuyumbisha, ama kukukwamisha, au kukuvurugia masiha, maana upole umebeba unyenyekevu ndani yake ! Yeremia 11:19 Lakini mimi nalikuwa kama mwana-kondoo mpole, achukuliwaye kwenda kuchinjwa; wala sikujua ya kuwa wamefanya mashauri kinyume changu, wakisema, Na tuuharibu mti pamoja na matunda yake, na tumkatilie mbali atoke katika nchi ya walio hai, ili jina lake lisikumbukwe tena.
Upole huu ndio uliomvusha Yesu ! Isaya 53:7 Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.

Kuna wakati adui ananuia kabisa kukukwamisha mahali kwa kuibua changamoto, ama vikwazo, ila ukiwa nao huo upole, utanyamaza kimywa na adui anakosa mwanya wa kukudhuru au kukuangamiza !
Sasa sababu ya maandiko kututaka upole wetu ujulikane na kila mtu ni ili kuwa na maisha ambayo Tunda hili litakuwa active au hai, ili kutuwezesha kunufaika nalo, usisahau kuwa anamalizia nakusema Bwan yu karibu, ikiwa na maana kuwa unapokaribia mafanikio kama Yesu, au kukutana na majibu yako, adui haachi kuleta vikwazo, iwe kwa ndugu, marafiki, muajiri wako, wafanyakazi wenzako,walezi na kadhalika akinui kukuzuilia kukutana na Bwana, sasa upole utakuvusha kama Yesu na Yeremia ! Ona haya maandiko :
Anaanza na kututaka tufurai, akiwa na maana upole umebeba ama hukuwezesha kufurahi, maana mazingira ya huzuni, na uchungu hayawezi kuzaliwa penye upole ! Alafu amani huyoke, kumbuja amani pia ni Tunda la Roho !, pamoja na Furaha ! Sasa ukipata upole, hayo mengine ni rahisi sana kuchipuza !
Wafilipi 4:4 Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.
:5 Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu.
:6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
7 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.

Katika somo hilo, tuna au una jigunza nini hapo ?

Natumai somo kuu, ni kwamba ukiwa mahali pagumu, huna majibu ya maswali yako, mazingira yanakuzalia ama hukutishia kukuzalia huzuni, au kukunyima amani, na furaha, masononeko na ukiwa zinakunyemelea! Basi upole ni dawa ! Ambapo utazaa Amani, na Furaha ! By Mwalimu Oscar Samba. Simu: +255759859287