Jumamosi, 3 Julai 2021
Mwalimu Oscar Samba THAMANI YA KUMKABITHI MUNGU MAISHA YAKO YA BAADAE na...
Jumanne, 6 Aprili 2021
Jumatano, 24 Machi 2021
Ujumbe huu ni sehemu ya #kitabu chetu cha MTUMIKIE MUNGU, UKubali #Wito, #Kuna Faida katika Kumtumikia Mungu, na Kuna Hasara za Kukaidi Wito.
Na Mwalimu Oscar Samba
Usipoelewa jambo hili, huwezi elewa ni kwa nini Mungu aliamua kumfuata Yona baharini! Angeweza kuamuacha na kuinua mtu mwingine!
Jumamosi, 6 Machi 2021
Muombee Elia ama Yusufu wako, Ni Msaada wa kutoka kwenye Majanga kama ya Corona. #Corona #Covd19
nA mWALIMU oSCAR sAMBA
Ujumbe huu ni sehemu ya #kitabu chetu cha MAMBO MUHIMU YA KUFANYA AU KUZINGATIA KUNAPOKUWA NA ADHABU YA KIUNGU INYOIJUMUISHA ENEO ULILOPO AU JAMII
Jumamosi, 27 Februari 2021
Kitabu chetu cha: MAMBO MUHIMU YA KUFANYA AU KUZINGATIA KUNAPOKUWA NA ADHABU YA KIUNGU INYOIJUMUISHA ENEO ULILOPO AU JAMII.
Na Mwalimu Oscar Samba
Neno Kiungu huwakilisha kutoka kwa Mungu au Shetani,
ujumbe huu ni sehemu ya hiki kitabu chenye mada na pwenti kadhaa, ila hapa
nimezicha,bua mbili tu; #Corona #Covd19 #Tsunam #Majanga #Kimbunga #magonjwayamlipuko #tanzania
1. Lifanye Eneo Unloishi kuwa Ghosheni yako. 2. Ijue
na Uitumie Damu ya Yesu ya Pasaka; 3. Mulize Mungu kama Daudi; 4. Litengenezee
Kusudi la Mungu Kisafina kama Musa, ama Nuhu; 5. Jifunze Jambo kwa Mke wa Lutu;
6. Sadaka kama Ulinzi; 7. Sadaka kama Sehemu ya
Rehema, Mfano ile ya Daudi kipindi cha adhabu ya Tauni, 8. Taka Kujua pigo Hilo
au Adhabu hiyo Inataka nini ili Ujisalimishe kwa Bwana, Mfano Rahabu, na Epuka
kosa la Farao.
9. Yajue na
Uyaombe Maombi ya Musa ya Kulitengeneza Boma, 10. Mtafute na Umuondoe Akani, 11.
Jitenge na Kusanyiko, au Kiunganishi cha Kusanyiko ama Waadhibiwa, ondoa jina
lako kwenye watu wanaotakiwa kupewa hiyo Adhabu kwa Damu ya Yesu.
12. Tafuta Maelekezo Maalumu ya Mungu juu yako, kama
Isaka dhidi ya Janga la Njaa na Wazazi wa Yesu. 13. Unapoisikia Hofu Usiipuzie,
Taaka Kujua ni Aina gani ya Hofu ala Uikabili..
14. Tafuta Kukumbuka kama Mungu Aliwahi Kukujuza
hapo Awali na Hukumsikia Vyema au Hukumbuki. (Amosi 3:7 Hakika Bwana MUNGU
hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.)
Sijui sana ni kwa nini kanisa la leo lina uzito kwenye hili, nijualo ni kwamba uwezo wa kusoma alama za
nyakati, au majira umekuwa ni adimu sana kwa kizazi cha leo! Nafahamu kuwa hali
ya kupuzia ndoto, kutokutambua jinsi Mungu anavyoongea, na mafundisho manyonge
kuhusu uhusiano wetu na Roho Mtakatifu ni miongoni mwa sababu ambatanishi.
Kama kuna mahali Shetani amefanikiwa leo ni kuondoa,
ama kuzimisha kama sio kufifisha karama ya unabii, na huduma ya nabii, pamoja
na neno la maarifa!
Na anatumia njia kuu kama mbili hivi, moja ni
kuhakikisha kanisa linapoteza imani na manabii au wanaotumiwa na karama hizi,
kwa kujiwekekea manabii wa uongo, ili kuwakatisha watu tamaa na kuwafanya wa
waone hata wale wa Mungu nao ni kama hao wengine!
Pili analitumia kanisa lenyewe, kwa kufikia hatua ya
kupinga, na kukataa, na kuzimisha huduma na karama hizi, na sababu zao ni
nyingi ila hazina hoja timilifu kibiblia, maana kama kuna wimbi la mafundisho
na huduma potofu, suluhu bado sio kuzima na kukataa ile ya kweli, bali wafunze
watu namna ya kutambua kweli na uongo. Mchele ukiwa na chuya, dawa sio kukataza
nyumbani wasipike tena mchele bali ni kuwafunza kuzitoa, na kama ni mcahanga
basi watake kuwa makini kuchambua maana mawe mengine ni yale meupe, kwa hiyo
yanafanana kwa karibu na mchele, lakini pia kama ni vigumu, wafunze kupembua au
kuuchambua wakati wanauosha na maji, njia ambayo ni salama zaidi.
Maharage yakiwa na mchanga au mawe, hayamwagwi, bali
huchambuliwa! Na wewe ukiona dosari katika hudumka na karama hizi, hakikisha
unazikabili!
Maandiki yako wazi kabisa katika biblia kuwa
tunatakiwa kujifunza na kuhakikisha kuwa tunasoma alama za nyakati, au tunajua
mabadiliko kwa kuzitambua dalili zake, mkulima asipojua kusoma uso wa nchi,
hakika atakuwa akipitwa na maamuzi dhabiti katika majira husika, wakati wengine wanandaa mashamba yeye atashindwa kufanya hivyo, ama atajikuta
akiwacheka wengine, maana kwa wengine ili walime ni hadi waone mvua imenyesha bila
kujua kwa kufanya hivyo ni gharama zaidi maana aridhi husumbua kwani kulima
kwenye tope ni kugumu zaidi! Pia ipo hatari ya kushindwa kufanya vyema maana
kuna uwezekano wa kunyeshewa! Kuna kuchelewa pia kupanda, maana wakati wa
kuotesha wewe ndo kwanza unakwatua udongo.
Jumapili, 17 Januari 2021
kitabu cha UKULIE WOKOVU

Jumapili, 1 Novemba 2020
MATESO, MAPITO SIO ISHARA YA KUPUNGUA, KUFIFIA AU KUTOKUWEPO KWA PENDO LA KRITO PAMOJA NAWE.
Na Mwalimu Oscar Samba.
Ujumbe huu ni sehemu ya kitabu chetu cha MUNGU ANAKUPENDA, chenye mukutadha wa kukujulisha hata katika taabu yako pendo lake lingali lipo hapo!
Wiki hii, (wakati
mada hii inaandikwa) nilimuliza Mwalimu anayetufundisha kitabu cha Matendo ya
Mitume swali gumu sana, ambalo lilisadifu ujumbe huu ambao ninauleta mbele yako
siku ya leo!
Nilimuliza ama
nalitaka kujua kuwa kweli ni Mungu huyu huyu liyejifunua kwa Stefano wakati anapiga
mawe! Stefano anasema anamuona mwana wa Adamu au wa Mungu katika mkono wa
kuume, tena tunaambiwa alikuwa amejaa Roho, kwa hiyo utatu mtakatifu ulikwepo
ukimtazama au uwepo wake ulikwepo pamoja naye!
Jumapili, 11 Oktoba 2020
MAJIRA YA KULISIMAMISHA JUA. Ni semu ya Hiki kitabu
Na Mwl Oscar Samba,
Lengo: Kukujengea Kiu ya
KuhakikihaMiujiza na Ishara na Matendo ya Mungu ya Ajabu Yanatendeka kwenye
Huduma yajo kama Ilivyokuwa Kipindi ca Baba, na Mababu Zetu Kiimani.
Utangulizi
Mungu wa ma
Mtendo ya Mitume ndie Mungu wetu! Wala hajawahi kubadilika, na jambo hili halitarajiwi
wala kutazamiwa kuwa ipo siku itakuwa vivi, maana imenenwa hivi; Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na
hata milele. Waebrania 13:8.
Ile ishara za Mungu hazijawa halisi kwako haina maana kwamba Mungu amebadilika, kaishiwa nguvu, ama amebadili utendaji na hata kufikiri kwamba ilikuwa ni kwa kipindi kile tu na kwa sasa haiwezekani, au inaonekana kwama Mungu hajaamua kufanya au kutenda kama hapo kale pia ni makosa tena mazito!
Jumapili, 27 Septemba 2020
MUNGU ANAKUPENDA KWA SABABU AMEANDAA MPANGO WA KUKUTOA KWENYE HILO JARIBU AU PITO.
Basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na
majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu. 2
Petro 2:9.
Wakati wana
wa Israeli wanalia, wanalalamika, wanaumia ama wanaonyesha hisia zao kutokana
na ugumu wa mateso yale ya nchi ya utumwa wa Misri, Mungu kwa upande mwingine
alikuwa akitekeleza mipango ya kuwaokoa kwenye ile nchi!
Hakuna mtu
aliyekuwa akiona, kutambua, au kufahamu kuwa upande wa pili Mungu alikuwa
akimpatia Musa maelekezo ya namna ya kuwatoa kwenye ile ncchi!
Na hata kabla
ya hapo, Mungu alikuwa akimuandaa Musa kwa ajili ya swala hilo, sio kwamba tu
alilifanya hilo wakati Musa akiwa Midiani, bali hata kabla ya Musa kukimbilia
huko Mungu alishamuandaa, ndio maana yale mahubiri yake kwenye kitabu kile cha Matendo
ya Mitume yanaelelezea vyema kuwa Mungu alimuandaa huyu, ila hakumuelewa
mapema, na wana wa Isreali hawakulielewa lile ndio maana walimkataa kwa wakati
ule!
Jumamosi, 19 Septemba 2020
Kitabu cha USIFIE JANGWANI Mwalimu Oscar Samba Pdf

Ijumaa, 28 Agosti 2020
Utangulizi wa Kitabu chetu cha UTUMISHI NA MTUMISHI
Mwalimu Oscar Samba
PENDO LA KRISTO JUU YAKO NI LA MAFANIKIO
Mpendwa nikutie tu moyo kuwa Yesu anakupenda, anakuwazia mawazo yaliyo mema, ni Mawazo ya Amani, Furaha, ana mipango mizuri juu yako, ni Mipango ya Kuinuliwa, Kufanikiwa, kama ilivyo nia yake katika 1 Yohana 3:2, kuwa anataka ufanikiwe kimwili au kifya na katika kila eneo la maisha yako ikiwemo uchumi, ndoa, huduma na kadhalika kama vile roho au nafsi yako ifanikiwavyo:
YESU ANAKUPENDA!
Na Mwalimu Oscar Samba
Sijui kama unajua kuwa Yesu anakupenda! Ni hatari kujaribu kusema kuwa mbona ninateseka, mbona maisha ni magumu, sasa inawezekanaje Yesu anipende wakati huu ni mwaka wa .. sijapona?
Ukweli ni
kwamba Yesu anakupenda, na kuteseka kwako ni wewe tu bado hujatambua unachotakiwa
kufanya ili kukubaliana na pendo hili! Unajua ndugu yangu acha nikwambie ukweli
huu, nikuweke wazi katika viwango hivi vya uwazi! Mungu ili afanye kazi kwenye
maisha yako ni lazima wewe umpe nafasi!
Mungu ni
tofauti sana na Shetani, Shetani huweza kulazimisha, anaweza kutumia hila na
mbinu batili ili kufanya jambo kwenye maisha yako, ila ili Mungu akusaidie wewe
unapaswa kumruhusu!
Mfano, kuna
mama mmoja alitokwa na damu kwa muda wa miaka 12; kwenye biblia tunajuzwa hili
jambo, muda wote huo alikuwa akiwaendea waganga wa kienyeji na matatibu wa dunia
hii! Ila siku alipoamua na kudhamiria moyoni mwake kwa kulishika pindo la vazi
la Yesu hapo hapo alipokea uponyaji, wake!
Sasa jionee!
Ni kwamba kupona kwake, kulitokea pale ambapo aliamua, alidhamiria kumuendea
Yesu; Luka 8:43 Na mwanamke mmoja,
ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa
mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote, 44 alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi
lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma.
Hapo pendo la
Kristo linadhibitika ndani yake! Uponyaji unatokea, lakini sio kwamba Yesu
alianza kumpenda alipomponya la! Upendo ulikwepo ila huyu mama alipoamua
kukubaliana na pendo hilo ndipo alipopona!
Yesu
alitupenda na alimpenda huyu mama hata kabla hajavaa mwili yaani hajaja humu
ulimwenguni, na pendo hili linadhibitishwa na Uungu wote; Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda
ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali
awe na uzima wa milele.
Dhambi
ilipoingia ulimwenguni pendo la namna hii ililijidhiirisha mara! Halikuanzia
katika kuzaliwa kwa Yesu, bali hata Agano la mlima Sinai ni ishara ya hili
pendo, Mungu alipochinja mnyama na kuwavika wakina Adamu nguo ilikuwa ni sehemu
ya utendaji wa hili pendo! Mahali pengine kwenye biblia hujulikana kama neema,
unapoona neema, uwe na hakika huwakilisha pendo la Kristo, tumeokolewa kwa
neema tu, ama tumeitwa kwa neema tu, uwe na uhakika ni pendo lake!
Pendo hili haliwezi
kujifunua kwako wakati ukiwa na shida unaenda kwa waganga wa kienyeji, ukiwa na
mahitaji humulezi Yesu unawaeleza watu tu na kuishia hapo! Hutaki kwenda
kanisani, maana huyu mama alimfuata Yesu kwenye kusanyiko, na penye kusanyiko
maana yake ni penye uwepo wa Mungu, sasa kwenye ibada ndipo alipo Kristo!
Usiende
kanisa ni kanisa, usiende kusanyiko ni kusanyiko, maana siku hizi watumishi
wengi wa uongo wameibuka, tafuta kanisa la watu walio hai kiroho, mahali ambapo
kiukweli hata akili na ufahamu wako wa kawaida unatambua hapo Mungu yupo, epuka
mbwe mbwe za Shetani, na misisimko isiyo na Mungu ndani yake.
Yawe ni
maombi yako na ni maombi yangu pia kuwa Mungu afunguwe macho yako ya ndani ili
uweze kujua sehemu sahihi itakayokuwezesha kukutana na Yesu wa kweli, maana siku
hizi kuna ma-yesu wengi wa uongo, hawamuhubiri Yesu mwenye kukemea dhambi, kwao
dhambi ni sehemu ya ibada, hapo kimbia!
Ukiona huduma
isiyokemea dhambi, hiyo imepotoka, ukiona huduma ambayo wazinzi na walevi wamo
humo humo na ni watumishi, hapo kimbia wala usiage! Ukiona mtumishi anawataka
washirika wake kimapenzi ujue huyo ni “ajenti” ama wakala wa kuzimu, na
ukimkubalia atakuunganisha na kuzimu moja kwa moja, kwani mashariti yao moja
wapo ya kuwaunganisha ni kulala na watu! Hususani wenye nyota ambazo
zitawasaidia kuvuta watu makanisani! Epuka na kimbia hili!
Unajua kuna
watu wanaenda kanisani ili kuirithisha nafsi yao kuwa nao wapo kanisani! Hii ni
hatari sana, ni sawa na kunywa maji machafu ili tu uwe umekunywa maji! Ni sawa
na kula mkapi au vyakula vibovu ili tu kukidhi hitajio la kula! Ukifikia hapo
upo mahali pagumu sana!
Maana baada
ya muda afya yako itakongoroka tu! Wengine huabudu kwa kufuata mkumbo! Yaani ni
mtumishi yupi anawika sana mjini siku za leo, akipoa au akiona ushabiki
umempungua basi hufikiri kuhama hapo! Akiibuka mwingine mjini, humfuata!
Watoto
hata! Shetani huwa naye anahubiri, tena ni muhubiri mzuri tu! Ukipinga muendee
Yesu kwenye Mathayo na Luka 4, utamuona Yesu akihubiriwa na Shetani pale, na maandiko
anamsomea, kuwa akiwa ndie Mwana w aAdamu ageuze jiwe kuwa mkate, na
alimuonyesha hata utajiri alionao akimpa na kanuni kuwa akimsujudia atampatia!
Sasa
usitishike na injili za mafanikio, maana hawakuanza wao alianza Shetani, na
kupata fedha au mafanikio kutoka kwao sio jambo la kigeni, maana hata Yesu angemsujudia
hakika angepewa, maana ni muhimu kujua nao huwa wanamsujudia nani!
Kusoma maandiko
na kuyafafanua siyo kipimo, kwani hata Shetani alimsomea Yesu, maana ni kweli
yapo kwenye biblia! La muhimu na jambo zuri kuliko yote ni wewe kuhakikisha
kuwa ndani yako unapata amani ya Kristo, maana wapo ambao Mungu anawakosesha amani
na mtu husika ila kwa ushabiki huzidi kugandamana naye! Huku ni kupotea!
Injili ambazo
jina la Yesu limewekwa kando, msisitizo wa maombezi sio katika jina la Yesu na
Damu yake kwenye uhalisia, ama nguvu za Roho Mtakatifu, bali ni katika
viambatanishi, au visaidizi, kama mafuta ambayo yamesingiziwa kuwa ya upako, na
wengi hawataki kujua kama ni upako upi unaotajwa hapo, maji ya upako au maji ya
baraka, wengine wanagawa hadi bangili za upako, pete za upako, nasikia siku
hizi kuna keki za upako, hii ni hatari
sana!
Najua wana
wa upotevuni ni wepesi sana kukinzana na ukweli huu, na wana hoja nyingi sana
wakitumia maanadiko, ila mioyoni mwao wanaujua ukweli, maana sifa zipo kwenye
mafuta na maji yakaniponya, Yesu amekuwa kama ni msaidizi!
Nisikilize,
ukitaka kuliona pendo la Kristo likikusaidia maishani mwako ni muhimu sana
kuhakisha kuwa unaambatana na Yesu kama alivyo, waepuke wanaokupa maji machafu,
katika Yohana 7:38-39 Yesu anaita akiwataka wale wenye kiu waje au waende kwake
ili awape maji!
Maji yake ni
safi, alimwambia yule mama kwenye kisima cha Yakobo katika Yohana 4 kuwa
kiyanywa hayo maji ya Yesu hataona kiu tena! Sasa wamekupa Yesu na bado kiu ya
ulevi ipo, wamekupa Yesu na bado una kiu ya kuiba waume za watu! Ukimuona mume
wa mtu mate yanakutoka kama fisi na mfupa! Wamekupa Yesu angali bado una kiu ya
dogo-dogo, ukimuona kijana “handsame” ama binti mrembo, hata kama ni umri wa mwanao
jicho linakutoka kama vile fundi simu aliyedondosha nati, maana nati zake ni
ndogo kwa hiyo asipotoa macho hawezi kuziona kirahisi, huu akiwa na hofu
usikute imepotea!
Unasema eti
umeokoka, au unamependa na una Yesu, sawa sikataii! Lakini mbona hajaondoa kiu
ya dhambi nadani yako! Bado ni mwizi, unazini kwa siri, nyumba ndogo kuacha
umeshindwa! Hakika huna Yesu aliyehai una yesu marehemu! Wala usinikunjie
ndita, ila ukweli ndio huo!
Anasema hivi;
Yohana 4:13 Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji
haya ataona kiu tena.
Yesu
akiingia nadani yako, na kiu ya mambo ya dunia ispoondoka, uwe makini, rejea msalabani
upya!
Neno la
Mungu ni maji, sasa injili kama inahubiriwa haibadilishi maisha yako, kuna mambo
mawili hapo makuu, wewe mwenyewe u na moyo mbovu, ama injili unayopewa ni maji
machafu, ni maji yasiyo na uwezo wa kukausha kiu ya dhambi, na tamaa zake,
swala la upinzani wa Shetani hili ni la maombi tu! Ila hatuwezi au maombi hayawezi
kukusaidia sana kama wewe mwenyewe hujakaa eneo salama, maana pepo mchafu
amtokapo mtu na akipata mwanya mwingine hurejea, maandiko husema mmekuwa safi
kwa lile neno, neno hukuweka kuwa safi, na mapepo hayakai maeneo ambayo
yamesafishwa kwa Damu ya Yesu!
Huwa nasema
kuna yesu aliyekufa, na kuna Yesu aliye hai, unaposema nataka kumuona Yesu,
nina haja na Yesu, uwe makini maana wakina Pilato wapo hapo kukupa yesu
aliyekufa kama Yusufu wa arimathayo, huyu alipewa Yesu/yesu ila mfu,
aliyempatia alihakikisha kuwa amekwisha kufa! Na aina hii ya Yesu hawezi kuleta
mabadiliko kwenye maisha yako!
Unasema una
Yesu lakini hatuoni badiliko la ndani; ndani yako, una sema una Yesu lakini
hatuoni matokeo ya wewe kuhuishwa hata kidogo! Yesu aliye hai, hukushindia
dhambi, huhuisha utu mpya na kuua ule utu wa kale, hawezi kuchangamana na
dhambi! Ukiona unajiita una Yesu lakini hakuna badiliko la dhambi au la kiroho
ndani yako uwe na hakika kuwa kuna shida ipo mahali, utakuwa wamekupa yesu
aliyekufa siyo Yesu aliye hai kama Yule aliyefufuka siku ya tatu, maana kuna
dini zina yesu sawa, ila ni yesu marehemu!
Wanahubiri
habari za Yesu, Lakini wao wenyewe ni wazinzi, ni walevi, hawawezi kusimama
madhabahuni bila kunywa pombe kidogo, hawawezi kukaa bila kutongoza washirika!
Ni mzee wa kanisa ila sigara anavutia chooni!
Ona hapa; Marko
15:44 Lakini Pilato akastaajabu, kwamba
amekwisha kufa. Akamwita yule akida, akamwuliza kwamba amekufa kitambo. 45 Hata alipokwisha kupata hakika kwa yule
akida, alimpa Yusufu yule maiti.
Kuna dini,
zimehakikisha kuwa yesu waliye naye amekwisha kufa, ndio maana wamekupa wewe!
Maji yao siyo yale halisi yenye uwezo wa kuondoa kiu ya dhambi, ndio maana
wamekupa wewe!
Huwa
ninaweka sana angalizo hili, kuwa unapokuwa na kiu ya kutaka kumjua Yesu,
unapokuwa na kiu ya kutaka kukoka, unapaswa kuwa makini tena mno, maana ukisema
nina kiu, moja kwa moja uwe na hakika kuwa wapo watu ambao hawaachi kukuletea
maji, ambayo kwa kweli siyo sahihi, ndio maanaYesu kwenye ile Yohana akapaza
sauti aksema kila mwene kiu na aje kwangu, aje anywe, hakusema na aje achote
maji ila alisema na aje kwangu, kwa hiyo jifunze kumtafuta Yesu kwanza, na sio
maji kwanza , kama wengi wafanyanvyo! (Maana ukiwa na Yesu, atakwambia haya
maji uliyopewa siyo yangu.)
Najifunza
sana kwa Yesu mwenyewe, alipokuwa pale msalabani na alipopatwa na kiu, alisema
naona kiu, na badala ya kumletea maji walimletea siki! Uwe na hakika na wewe
ukisema nina kiu, wapo na watu ambao nao watakuletea siki ama maji machafu!
Ukisema
nataka kuokoka, ninamtaka Yesu watakwambia usiondoke kwenye dini yetu maana na
huku pia watu wanaokoka, kuna vikundi huku nako vya uaomsho, uwe na hakika ni
uamsho bandia, maana kuna na moto bandia, ambao hufananishwa na ule wa Roho
Mtakatifu!
Namtaka
Yesu, wanakuletea Yesu ambaye amekufa, hawezi kuondoa dhambi! Ndio maana adui
ameweka utitiri wa madhehebu na makanisa mapya na watumishi wengi, ni ili kuwapoteza
watu, maana ma-yesu wafu wamejaa sana humu duniani! Umakini unahitajika sana!
Asante kwa
kunisikiliza (nafsini mwako), ama kunifuatilia kwa njia ya usomaji huu wa hii
makala, nina amini kuwa kuna kitu umekipata hapa, Yesu anakupenda, ila kama
hujakutana na pendo lake uwe na hakika kuna dosari ipo mahali, chukua hatua
mapema mnoo!
Pia anasema
kwamba mtu akimpenda atazishia amri zake, kwa hiyo kama kweli umedhamiria,
mpende kwa kuzishika amri zake, epuka michanganyo, epuka kuuzoelea wokovu,
asante na Mungu akubariki mno; Yohana 14:23
Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba
yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. 24 Mtu
asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu,
ila ni lake Baba aliyenipeleka.
Hongera kwa
kusoma ujumbe huu, nakutia moyo kuzidi kumtazama Mungu, na pia uwenda
hujaokoka, yaani Yesu sio Bwana na mwokozi wa maisha yako! Nakutia moyo tena
kuokoka sasa! Yamkini ni uchumi, fedha, hazipatikani, unazingirwa na nuksi na
mikosi, kila unalofanya haliendi, unakabwa na mapepo, ! Wewe njoo kwa Yesu na
hayo yote yatapita kabisa ! Sasa natumi u
tayari!
Sema; MUNGU
BABA, NINAKUPENDA, ASANTE KWA KUNIPENDA KWANZA, LEO NIMETAMBUA KUWA MIMI NI
MWENYE DHAMBI, NA NIPO TAYARI KUOKOOKA, TAFADHALI INGIA NDANI YANGU, SAMEHE
DHAMBI ZANGU, NA FUTA JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKU, NA ULIANDIKE SASA
KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE, Ameni.
Kwa kufanya
hiyo umekwisha kuokoka sasa, na tafadhali tafuta kanisa la watu waliokoka
lililopo karibu nawe ukasali, hapo, waambie kuwa umeokoa hivi karibuni, ili
wakulee vyema kiroho.
Mawasiliano
yetu, kwa M-Pesa au Simu: +255 759 859 287, barua pepe:
ukombozigospel@gmail.com
pia
temnbelea: www.ukombozigospel.blogspot.com
.
Alhamisi, 25 Juni 2020
UWE HODARI, SHUJAA NA MOYO MKUU.
Jumamosi, 20 Juni 2020
Usizike Ndoto Zako.
Alhamisi, 4 Juni 2020
NGUVU YA MAOMBI YA KUOMBA BILA KUKOMA
Ijumaa, 27 Machi 2020
Mwalimu Mwakasege Atoa Wito wa Kushiriki Maombi Dhidi ya Ugonjwa wa Korona
Bwana Yesu asifiwe.
Hili ni ombi kwa kila aliyewahi kuhudhuria kongamano letu,la maombi la kitaifa, tunalofanyia Dodoma kila mwaka. Lakini,hata kama hujawahi kuhudhuria kongamano hilo-ombi hili linakuhusu pia.Tunajua umekuwa ukiombea tatizo la ugonjwa wa 'Corona'. Pamoja