Jumatatu, 15 Mei 2017

EPUKA KUYAFANYA HAYA PUNDE UMUONAPO MUNGU YUPO KIMYA.

Kijana mmoja akasema, “Sitowi tena sadaka maana kila nikitoa ndo kama matatizo yanaongezeka”
Wengine wameanguka kwenye uzizi na uasherati huku sababu ikiwa ni kumuona Mungu kama awasikii ama amechelewa kuwaletea majibu yao, aidha ya kuolewa ama mtoto.
Sarai akamwambia Abrahamu/Ibrahimu, “Basi sasa, Bwana amenifunga tumbo nisizae, umwingiliye mjakazi wangu, labla nitapata uzao kwa yeye.” Abrahamu akaisikiliza Sauti ya Sarai. Mwanzo 16:2.

Baada ya hapo kilichofwata ni Ibrahimu kuzaa na kijakazi huyo wa bibi Sarai na hatimaye kumpata Ishmaeli ambaye

MUNGU ANAPOKUWA KIMYA FANYA YA FWATAYO. Sehe. 2.

Inaumiza kuwa katika pito gumu na unamtumaini Mungu kisha kumuona Yupo kimya, Ingawaje wakati mwingine huongea ila hatuelewi ila kiukweli upo wakati anakuwa kimya kama wakati ule wa Yesu pale msalabani.

Wengine hujifariji kuwa alinyamza kwa sababu Yesu alikuwa amebeba dhambi na Mungu hachangamani na wenye dhambi. Hoja hii kwangu ni dhaifu kwani kama aliweza kuzungumza na Petro katikati ya dhambi yake ya kumkana Yesu kwa ishara ya jogoo kuwika huku Yesu akimgeuki na kumkumbusha moyoni maneno yale ya kwamba kabla ya jimbi kuwika atamkana, alishindwaje kunena na mwanaye aliyemtuma kwa kusui hilo?

Ila katika yote hayo haipaswi kukata tamaa ama kutafuta njia za mkato kama wengine wafanyavyo baada ya hali kama hii.

MUNGU ANAPOKUWA KIMYA FANYA YA FWATAYO. Seh. 1


Ni rahisi kunena kinyume na mtazamo huu ya kwamba Mungu hawezi kunyamaza ila wasomaji wa maandiko na watu wanaopitia mapito magumu na ya muda mrefu ni wepesi wa kukubaliana na Falisafa hii.

Ila kumbuka hali hii ilimkuta hata Yesu, “Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?”, Mathayo 27:46. Kiukweli Mungu alikuwa Kimya. Hatumuoni akiongea naye wala kumjibu lolote baada ya kukamatwa kwa Yesu.
Kuna taswra kuu mbili za Mungu kunyamaza kimya, ya kwanza ni ile ya mtu kutenda dhambi na Mungu kumuacha, na ya pili ni ile ya mtu kuwa katika hali ya pito huku Mungu akipima subira yake iliyondani ya Saburi ya Kimungu ama Mungu akimsubiria achukuwe hatua fulani ndipo amjibu.

YASIYOWEZEKANA KWA WANADAMU KWA MUNGU YANAWEZEKANA.

Mwalimu Oscar Samba
Uhali gani mpenwa mwenzangu katika Bwana? Natumai u buheri wa afya.

Leo nimekuandalia ujumbe mahususi kwa ajili ya kukujuza ukubwa na Uweza wa Yesu Kristo katika mambo yaliyoonekana ni magumu kama mlima ama bahari katika maisha yako.

Ni kweli hitaji ama jambo lilopo mbele yako ni kubwa kuliko wewe na hata mimi mwenyewe ni kweli siliwezi, ila Yesu tunayemuamini analiweza. Amini tuu kama alivyomwambia dada yake na Lazaro rafiki yake kuwa anapaswa kuamini tu.

MTAZAME NYOKA WA SHABA.

Ndugu yangu, wasalamu katika Bwana Yesu Kristo, Ewe unayepita katika mapito magumu usifadhaike wala kukata tamaa badala yake mtazame Yesu kama Nyoka wa Shaba.
Kama Musa alivyomuinua yule nyoka wa shaba jangwani ndivyo Mwana wa Adamu hanabudi kuinuliwa.”
Katika maandiko matakatifu yaliyopo kwenye kitabu kile cha Hesabu yanaitaja nyoka ya shaba kama ishara ya ushindi katika nyakati zilizo ngumu kimaisha. Kwani kipindi hiki wana wa Iziraeli walikuwa wakiumwa na nyoka wa moto ama wenye sumu kali na walipoteza maisha punde.
Ila Musa alipata maelekezo kutoka kwa Mungu ya kwamba ainuwe nyoka ya shaba kwa kuitundika juu ya mti na kila aliyeng’ata na nyoka ya moto alipomtazama nyoka huyu alipokea uponyaji.
Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti: hata ikiwa nyoka amemuuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya sahaba, akaishi”.Hesabu 21:9.
Nami leo hii ninakuta kutokukata tamaa ama kuacha WOKOVU kwa sababu ya ugumu wa maisha ama mateso kwenye ndoa, uchumi ama biashara kuwa ngumu, magonjwa, kukataliwa au vita kwenye ulimwengu wa roho.
Bali inua macho yako ya Imani na kwa Imani; umtazame Yesu aliyeinuliwa kwenye ulimwengu wa roho kama yule nyoka wa shaba jwangwani na hakika hapo utapata majibu yako.
Kumbuka walioshindwa kumtizama yule nyoka wa shaba walipoteza maisha yaani walikufa hali iliyowafanya washindwe kufika Kanani. Na wewe ukilitazama tatizo lako utakwama maana ni kubwa kuliko wewe bali mtazame Yesu aliye dawa ya tatizo lako nawe utashinda, tena na zaidi ya kushinda.

Na Huduma ya UKOMBOZI GOSPLE, Arusha Tanzania, Kwa maombi, Ushauri, Maswali au Sadaka wasiliana nasi, Barua pepe: ukombozigosple@gmail.com Simu: +255 759 859 287 pia waweza itumia kwa M-PESA. Zaidi www.ukombozigosple.blogspot.com

Jumapili, 7 Mei 2017

Mwalimu Oscar Samba KUKAA KWENYE NAFASI

Mwalimu Oscar Samba, MAMBO MUHIMU KATIKA KUMTUMIKIA MUNGU

Wanafunzi wa Vyuo na Shule, Usimwache Yesu mfikapo vyuoni/Shuleni

Mwalimu Oscar Samba
+255 759 859 287  Kumekuwa na wimbi kubwa la wanafunzi kuyaacha maadili ya kikristo pindi wa fikapo shuleni ama vyuoni.

Jambo hili ni hatarishi kwao kwani mazingira ya masomo hufananishwa na eneo la kivita kwenye ulimwengu wa roho. Katika maeneo kama haya ndipo hujitokeza wanafunzi waliozoezwa kutumia ushirikina au wenye ujuzi katika mambo hayo. Na wewe ukiyumba kiroho maana yake ni kwamba utashindwa na mambo hayo na kujikuta ukididimia kiroho na kimwili huku maono au ndoto zako zikikwamia njiani.

Pia wachawi na waganga wa kienyeji ama washirikina hupenda kudhuru maeneo hayo kwenye ulimwengu wa roho ili kuiba nyota za wanafunzi, kuwachezea ama kuwatumikisha kichawi na hata kujipatia wajumbe wao hapo.

Ndio maana katika maeneo ya mashule ama yvuo hakuishi vituko vya kishirikina hususani kwenye vyoo na hata mabweni. Ukiwa na Yesu utayashinda haya kirahisi na wewe hawatakuweza.

Na sababu zifwatazo ndizo huwafanya wanafunzi wengi kumuacha Yesu punde wafikapo katika mazingira kama haya; 
1. Kufwata mkumbo, wanafunzi wengi hujikuta wakifwata mkumbo kwa kuiga mambo yasiyofaa, ikiwemo vitendo vya ulevi na hata ukahaba. Pamoja na mavazi.

2. Kukosa ujasiri wa kumtaja Yesu ama kuona wokovu kama ni aibu, Nisikilize kwa bidii ili upone, Yesu sio mzigo wala sio aibu kuwa naye bali ni sehemu ya Ushindi. Kumbuka msalaba kwao wapoteao ni upuzi bali kwetu siye ni ushindi, uzima, na nguvu tele maishani mwetu. Usikubali kuona haya kumtangaza Yesu maana anasema atakayemkana mbele ya watu naye atamkana mbele ya Baba.

3. Kuwa na marafiki waovu, siku zote rafiki wa mtu ni mtu, na unapojifanyia marafiki wasiofaa ni kwa uaribifu wa nafsi yako na maisha, na maono yako kwa ujumla. Mithali 18:24a Ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa uaribifu wa nafsi yake.. 
Mithali 22: 24 Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi, wala usiende na mtu wa gadhabu nyingi.

Bibilia inatupa muongoza sahihi wa namna ya kuwa na marafiki kwani ukiwa na rafiki mwizi na wewe utakuwa kama yeye, aliye kahaba ama mwenye tabia ya kuchuna wanaume "Mabuzi" ama mwenye macho ya kutamani mabinti, "Mademu" hakika na wewe utafanana naye. 
Katika hili ninakuta kuwa makini sana na marafiki, ingawaje dhumuni langu sio kukunyima kushirikia nao kimasoma, ila shabaha yangu ni kukuondolea ukaribu nao.

4. Kuwa na gelifrend au Boyfrendi, Kitendo hiki cha mwananfunzi kuamua kuwa na mpenzi kabla ya wakati wa kibibilia ama nje ya mpango wa kimungu ni dhambi na jambo hili hufungua mlango kwa Shetani unaomuwezesha kunyonya hali yako ya kiroho polepole na kujikuta ukianza kuwa na Wokovu wa mazoea ama wa kidini na hatimaye kuwa debe tupu litoalo upatu. 

Usidanganywe eti huo ni uchumba, hii ni hila ya Shetani kwani uchumba wakibibilia haufanyiki hivyo, na huwa na utaratibu ufwatao , Mchungaji wako ajue, Wazzzi wafahamishwe, kisha mchakato wa mahari ufanyike na utangazwe kanisani.
Kama hayo hayajafanyika ama hakuna rathi hiyo fahamu kuwa mpo mtegoni.
Na huku ni kumkosea Mungu Mpendwa, Wimbo uliobora 3:5 Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, kwa paa na kwa ayala wa porini: msiyachoche mapenzi, wala kuyaamsha, hata yatakapoona vyema yenyewe.

Ndugu yangu kiimani ninakutaka kumshika Yesu kwa bidii unapokuwa katika masomo yako na endelea na misingi ya kiroho ili kufanikiwa vyema. Usikubali kuwa mlokole ukienda likizo ila kibaka ama mwizi au mtukanaji ukiwa shueni. Achana na utamaduni wa kumwa mwema mbele ya wazazi ila muovu mbali ya upeo wa macho yako.

Swala la kiroho ni lako wewe na Mungu wako. Wakina Meshaki, Shedraki na Aberinego na Danieli walipofika uamishoni kule Babaeli na kuingizwa katika iamaya ya kifalume huku wakipelekwa darasani ili kuijua lugaha ya wazawa na maarifa ya kifalume kwa shabaha ya utumika kwa mfalume Nebukadreaza hawakumwacha Yesu; Badala yake waliongeza bidii na hatimaye Mungu wao kutukuzwa hapo.

Na wewe hapo ulipo inahitajika Mungu wako atukuzwe na kila mtu amptambuwe huyo uliye naye kama wakina Meshaki na Aberinego, Shedraki na Danieli kipindi kile. 

Pia kama hujaokoka fanya hima umpokee huyu Yesu kwani ndiye atakayekuwezesha kuishi maisha mazuri chuoni maana bila Yeye wachawi, walozi na wasoma nyota wanaweza kukuibia mafanikio yako na kujikuta unafukuzwa shule bila sababu za msingi ama kuishilia kwenye vitendo vya ulevi na ukahaba na hatimaye kuvurugikiwa maishani.

Kumbuka kuwa sio kila anayetenda mambo ya ajabu ama maovu vyuoni ama mashuleni amependa bali wengine wamelogwa au kuchezewa kwenye ulimwengu wa roho na watu wenye husuda, wivu na hata wenye nia mbaya. Wapo walioibiwa nyota, na waibao hutupa tabia za ulevi, ukahaba ama mwenendo mbaya pia magonjwa ili mshuhulike na hayo badala ya kugundua wizi huo wa nyota ama huwa kama bumbuzi kwa kutokuja kuwa ameibiwa.

Yesu pekee ndiye awezaye kumuweka huyu mtu salama,

Kama huja Okoka na unataka kuokoa ama ulikuwa umeokoka na ukalega kiroho ama wakati huu upotayari kurejea tafadhali fanya sala hii ya toba.

Sema, Mungu Baba, nipo mbele zako, Nimetambua yakuwa mimi ni mwenye dhambi, Na nipotayari kukufwata, Na ninakuamini na kukupokea kama Bwana na Mwokozi wa maisha yangu, ninakupenda Yesu, nilinde kiroho na kimwili. Ameni .

Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la kihoho mahali ulipo ukaabudu, Ameni.

Na Huduma ya Ukombozi Gosple, kwa maombezi ama ushauri na sadaka Ya M-pesa tumia +255 759 859 287.  


USIFIYE JANGWANI MPENDWA

Na Mwalimu Oscar Samba
Ndugu yangu mpendwa katika Bwana ninakutaka kutokukata tamaa na maisha ya wokovu, kwani haijalishi ni jambo gani unalolipitia, mbele upo ushindi.

Wana wa Iziraeli walisafiri kutoka nchi ya utumwa ya mateso ya Misiri ili kuelekea nchi ya Maziwa na Asali kama Bwana alivyo waaidia, ila iliwalazimu kupita jangwani. Haikuwa safari nyepesi kutokana na ugumu na manthari ya Jangwa.

Ila wale walioshinda walifanikiwa kuingia Kanani na hatimaye kuyaishi maisha yale ambayo Mungu aliwaaidia. Na wewe yakupasa kushinda.

Ijumaa, 5 Mei 2017

Wasifu, Mjuwe Mwalimu Oscar Samba.

Mwalimu Oscar Samba
Ni Mwalimu wa Neno la Mungu na Muasisi wa Huduma ya Ug, yenye kirefu cha UKOMBOZI GOSPLE. Na yenye tafsiri ya Injili ya Ukombozi.

Pia ni mwandishi wa vitabu vya Neno la Mungu, na kitaaluma ni mwandishi wa habari mwenye elimu ya ngazi ya Diploma/Stashahada na ngazi ya Cheti cha Juu. Amesomea kwenye chuo cha AJTC kilichopo mkoani Arusha.

Ana elimu ya Thielojia ngazi ya cheti aliyoipata kwenye chuo cha kupanda makanisa Makuyuni mkoani Arusha kikiwa ni tawi la chuo cha TAG cha BIBILIA ARUSHA, kwa hivi sasa ni Chuo cha Bibilia Kanda ya Kasikazini.

Pia amehitimu shule ya Msingi Maharo na ya sekondari ngareni zilizopo mkoni Kilimanjaro. Kabila lake ni mchaga wa maeneno ya Rombo. Na Dini yake ni Mlokole.

Baba yake ni Prospa, Mama yake ni Flora. Na Ukoo wake ni Samba.  Ni mtoto wa pili katika familia ya Mzee Prospa.
Kuzaliwa ni 6/6/1989,
Anaishi mkoani Arusha na kiasili ni mtu wa mkoani Kilimnjaro.

Pia Kabla ya kuingia kwenye wito wa kitumishi aliwai kufanya Siasa na alikuwa mwanachama wa vyama viwili ambapo chama cha kwanza alikitumikia kwa muda mrefu zaidi na hatimaye kuhamia kingine kutoka na masilai ya kisiasa.

KUTOA MIMBA NI DHAMBI

Na Mwalimu Oscar Samba
Kumekuwa na matukio mengi ya watu kutoa mimba huku baathi yao wakijifariji kuwa kufanya hivyo sio mauaji.

Ninataka kukufahamisha bayana ya kwamba utoaji wa mimba ni mauaji, na kibibilia hakuna muuaji mwenye uzito zaidi ila ukubwa ama kipimo cha kosa hilo la umwagaji damu ni sawa.

Yaani aliyeua mtoto aliyetumboni na aliyeumuua mtu wa miaka kumi ama zaidi wote hukumu yao inalingana.

Kwa kifupi aliyetoa mimba na aliyeshiriki wote ni kundi la wakina kaini.

Ikumbukwe kuwa kibibilia mtoto ama mtu hutambulika toka tumboni, Na hapo Mungu umuhesabu sawa na aliyezaliwa.

Ndio maana akamwambia Yeremia kuwa "Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa..." Yeremia 1:5

Yohana mbatizaji alicheza akiwa tumboni mara baada ya mama yake kukutana na mama yake na Yesu. Hii ni ishara kwamba kusudi la Mungu lilidhirishwa ndani yake angali tumboni mwa mamaye, sanjari na hapo kwaYeremia.

Kwa hiyo epuka kushiriki dhambi hii kwa namna ya aina yoyote ile na kama ulishashiriki tubu haraka.

USIKATE TAMAA YESU ANAWEZA

Mwalimu Oscar Samba
Yaliyoshindikana kwa wanadamu, Kwa Yesu yote yanawezekana.

Hivyo ndugu yangu ninakutaka kutokukata tamaa na maisha kwa namna ya aina yoyote ile kwani Yesu anayaweza yote.

Yeye aliyefanya njia kwenye bahari ya Shamu atafanya njia pia katika mapito yako.

Yeye aliyemfufua Lazaro, aweza fufua leo Uchumi wako, Ndoa yako na hata kukurejeshea afya yako.

MAOMBI YANGU KWAKO:
Mungu wangu na akuponye na magonjwa yako yote na kukuondelea mateso yako leo. Amen.

Mwalimu Oscar Samba, MTUMAINI BWANA KATIKA PITO LAKO

MWALIMU OSCAR SAMBA NAFASI YA IMANI KATIKA MAISHA YA UOKOVU

Jumatano, 3 Mei 2017

Nukuu iliyopo kwenye Kitabu cha Sadaka Kama Mbegu cha Mwalimu Oscar Samba

 "Ni jambo la hatari sana kufikia hatua ya kula Sadaka ambayo Mungu amekupa kama Mbegu na umejua fika kabisa alikupa kuitoa ila kwa sababu una hitaji fulani ukalazimika kuitumia. Nisikilize kwa ukaribu na utulivu: Maana hitaji na uhiitaji wa mwadamu hauishi, na Mungu anapotaka umtolee Sadaka kama Mbegu haimaanishi kuwa haioni shida yako, laa! Asha! Anaiona na amepanga kuitatua kwa kukupa njia ya upandaji.
Hivi kama una uhitaji wa mahindi kilogramu 30 na una mbegu ya mahindi kilo mbili. Itakufaidia nini kula mbegu hizo leo na kubakiwa na uhitaji wa kilogramu 28? Ni ya heri kuzifukia mbegu mchangani kama Yesu alivyosema kwenye Mariko 4:26-29. Na hatimaye kukupatia mavuno yatakayokidhi mahitaji yako.
Masikini wegi ni masikini kwa sababu walikwepa garama za kutoka katika umasikini. Na matajiri wengi ni matajiri kwa sababu walikuwa majasiri wa kuzikabili gharama za kutoka katika umasikini huku wakiwa wanajua faida za kuwa tajiri.
"